Simba, Yanga SC zatoshana nguvu

Leo Novemba 7, 2020 mechi kabambe iliyokuwa inasubiriwa kwa shauku na mamilioni ya Watanzania kati ya watani wa jadi Simba SC na Yanga SC imemalizika kwa kwa matokeo ya 1-1, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Matokeo hayo yanazidi kuwaacha nyuma mabingwa watetezi Simba SC chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck, licha ya kuwa na kikosi klichojaa nyota wengi wa ndani na nje.

Katika mchuano huo, Yanga SC imeanza kupata bao la kwanza kupitia kwa Michael Sarpong 31' kwa penalti baada ya Tusisila Kisinda kuchezewa faulo nje kidogo ya 18 na nyota, Joash Onyango na mwamuzi Abdalah Mwinyi Mkuu kuamua ipigwe penalti kipindi cha pili.

Aidha, Yanga SC kipindi cha pili walianza kwa kasi ila beki kisiki Lamine Moro alishindwa kumaliza 90' baada ya kupata maumivu ya goti.

Nafasi yake ilichukuliwa na Said Juma ambaye alishuhudia bao la kwanza kwa Simba 86' kwa pasi ya Luis Miquissone ambaye alikuwa ni mwiba kwa wapinzani.

Hata hivyo, matokeo hayo yanaifanya Simba SC kubaki nafasi ya tatu ikiwa na alama 20 huku Yanga ikiwa nafasi ya pili na alama zake 24 na vinara ni Azam FC na alama zao ni ishirini na tano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news