Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai amewaapisha wabunge wawili walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anaripoti Mwandishi Diramakini
Wabunge walioapishwa leo Novemba 30, 2020 ni Mheshimiwa Humphrey Polepole na Riziki Said Lulida, zoezi ambalo limefanyika katika viwanja vya Bunge.
Baada ya kuwaapisha wabunge hao wawili, Ndugai amesema wabunge 19 Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao pia wamevuliwa uanachama na chama hicho ni wabunge halali na kwamba yanayoendelea ndani ya chama hicho, hayo ni ya kwao wao CHADEMA.
Wabunge wa Kuteuliwa na Mheshimiwa Rais, Mhe. Riziki Lulida na Mhe. Humphrey Polepole wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge Mhe.Job Ndugai na Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai mara ya kuapishwa kwenye viwanja vya Bunge hii leo Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge).
Wabunge hao ni Halima Mdee,Asia Mohamed, Felista Njau, Naghenjwa
Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Simon, Anatropia
Theonest,Salome Makamba, Conchester Lwamraza, Grace Tendega, Ester
Matiko,Secilia Pareso,Ester Bulaya, Agnes Kaiza, Nusrat Hanje, Jesca
Kishoa, Hawa Mwaifunga na Tunza Malapo
"Wabunge wote
walioaapishwa ni wabunge halali wakiwemo wa CHADEMA, nashangaa
wamewafukuza hao wabunge 19, hayo yanayoendelea ni ya kwao. Tutawapanga
wabunge wote kwenye kamati kulingana na sekta zao zinapoangukia,"amesema
Spika Ndugai, huku akiwataka waandishi wa habari kuwa na weledi kuhusu
shughuli za Bunge na kuepuka kuwa sehemu ya upotoshaji.
Polepole na
Lulinda wameapishwaa baada ya kuteuliwa na Rais Dkt.John Pombe Joseph
Magufuli kupitia nafasi 10 ambazo Katiba imempa nguvu ya kufanya hivyo.
Mbunge wqa Kuteuliwa na Mheshimiwa Rais, Mhe. Riziki Lulida akila kiapo mbele ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai katika viwanja vya Bunge hii leo Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge)
"Kwa
hiyo wale waliokuwa na wasiwasi sijui kuna nini na nini, wala nawaambia
wasiwe na wasiwasi wale ni wabunge kamili.Ninawaomba Watanzania wote
tupige vita ukandamizaji dhidi ya wanawake kwa kisingizio
chochote,"amesema Spika Ndugai huku akionyesha kushangazwa na Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akisema
amepigwa chini na ni mzoefu wa kuanguka.
"Kwa mtu mzima na
mwanaume wa Kitanzania ni aibu kubwa kutukana wanawake. Nimuonye (Mbowe)
wanawake ni mama zetu na ni dada zetu, hata pale wanapokuwa wamekosea
sio kuwafukuza kama vibaka," alisema Spika Ndugai na kuongeza. Lakini
yupo mwanamke alikuwa anagombea kule Morogoro amesimama na kuwaita
wenzake ni COVID 19, unaona kuwa safari ya wanawake ni ndefu. Hamjui hao
wanawake 19 wamepita mapito gani, vipo vyama ni kampuni za watu, yaani
wanawaburuza kama wanavyotaka,"amefafanua Spika Ndugai.
Spika
Ndugai amesema kuwa, "hao ni wabunge, hawawezi wao na genge lao la
wanaume wakafanya hivyo dada zetu, lazima ubaguzi wa kijinsia upigwe
vita na kila Mtanzania. Mbowe umesahau, Halima Mdee alivyovunjika mkono
kwa ajili ya kumfuata gerezani. Esther Bulaya alipigwa hadi akazimia
akalazwa hospitali kwa ajili yake, Ester Matiko amelala gerezani kwa
ajili ya kumpigani, lakini mshahara wao ni kuwafukuza bila kuwasikiliza.
Mbunge wa Kuteuliwa na Mheshimiwa Rais, Mhe. Humphrey Polepole akila kiapo mbele ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai katika viwanja vya Bunge hii leo jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge).
"Haiwezekani,
analalamika mwanachama wao Nusrat ambaye alikuwa mahabusu. Analalamika
kwa nini ametoka mahabusu,awe ametoka usiku au muda gani ili mradi
ametoke wewe unachotakiwa ni kushukuru Mungu, ndiyo maana tunasema
baadhi ya hivi vyama ni shida."
Katika hatua nyingi Spika Ndugai
amekemea vikali watu wanaobeza sehemu zinapofanyikia shughuli za Bunge,
huku akifafanua kuwa zinaweza kufanyika sehemu yoyote eneo la Bunge
ambalo Spika wa Bunge ataona linafaa.
"Wapo rafiki zetu ambao
hivi karibuni wamejipambanua kukejeli shughuli za Bunge. Ni
watahadharishe kuwa sio sawa kwa mtu yeyote kukejeli shughuli za Bunge
hata wabunge waliokwishakuapishwa.
Tags
Habari