TAKUKURU yaokoa mamilioni ya fedha

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) mkoani Ruvuma katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Septemba imefanikiwa kuokoa fedha zaidi ya shilingi milioni 107,478,845 kutokana na chunguzi mbalimbali ambazo imezifanya, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma, Hamza Mwenda amesema kuwa, katika kutimiza moja ya majukumu yake taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walifanikiwa kuokoa kiasi hicho cha fedha.
Ameeleza kuwa, shilingi 488,000/= zimepatikana kutokana na marejesho ya madeni ya Benki ya Wananchi Mbinga (MCB) fedha ambazo ziliwekwa kwenye akaunti ya Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru iliyopo Benki Kuu Tanzania (BoT).

Ameeleza kuwa, shilingi 94,420,845 zimeokolewa kutokana na uchunguzi unaoendelea katika vyama vya kuweka na kukopa wilayani Songea na shilingi 1,436,000 ni marejesho ya madeni ya Muungano SACCOS ya wilayani Namtumbo.

Amesema kuwa, shilingi 2,465,000 ni marejesho ya madeni ya Mbinga Teachers SACCOS na shilingi 1,779,000 ni marejesho ya madeni ya Mbinga Kurugenzi SACCOS ambapo fedha zote za SACCOS ziliwekwa kwenye akaunti za vyama husika.

Amefafanua kuwa, shilingi 5,890,000 ni fedha iliyookolewa wilayani Nyasa kwenye deni feki alilowekewa Ufunuo Chirwa na mtu wa Taasisi ya Maboto kwani mkopaji alistahili kulipa shilingi 4,000,00 lakini aliwekewa deni la jumla ya 9,890,000 kwa njia za ujanja ujanja.

Mkuu huyo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano na TAKUKURU katika mapambano ya kupinga rushwa kwa kukemea, kuzuia vitendo vyote vyenye viashiria ya rushwa katika jamii na kwenye ofisi za umma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news