TAKUKURU yaonya walimu, wasimamizi wa mitihani

Walimu na Wasimamizi wa Mitihani mkoani Njombe wametakiwa kuacha kushiriki vitendo vinavyoashiria utoaji wa rushwa katika kipindi cha Mitihani ya Kidato Cha Nne na cha Pili inayotarajiwa kufanyika siku za usoni hapa nchini,anaripoti Mwandishi Diramakini.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rusha (TAKUKURU) Mkoa wa Njombe, Kassimu Efreim wakati taasisi hiyo ikitoa elimu kwa klabu za wapinga rushwa zilizoundwa katika shule mbalimbali mkoani hapa zenye lengo la kukemea vitendo vya rushwa.

"Tunaomba sana wasimamizi wa mitihani zingatieni sheria, kanuni na taratibu, usimamizi wa mitihani ya serikali tunategemea kusiwe na ushawishi wa rushwa na TAKUKURU tupo,"amesema Mkuu huyo wa TAKUKURU.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Njombe,Kassimu Efreim akizungumza na wanafunzi wa klabu za wapinga rushwa (hawapo pichani) zilizoundwa katika shule mbalimbali mjini Njombe.
 
Kwa uapnde wake, Mwalimu Sreven David Mwakila kutoka Mpechi Sekondari pamoja na Mwalimu Adbelta Mgaya wanasema kuwa, wamekuwa wakitoa elimu kwa wanafunzi juu ya madhara ya rushwa huku wakitaja madhara yenyewe na namna yanavyoathiri jamii.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa makini kusikiliza elimu kuhusiana na namna ya kuzuia na kupambana na rushwa kutoka kwa Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Njombe, Kassimu Efreim (hayupo pichani).
Walimu wakiwa makini kumsikiliza Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Njombe, Kassimu Efreim (hayupo pichani) wakati akitoa elimu kuhusiana na namna ya kuzuia na kupambana na rushwa.
 
 "Tunaweza tukapata wataalamu ambao hawajakidhi vigezo, lakini vile vile uchumi wa taifa unaweza ukadidimia mfano zikajengwa barabara mbovu na mwisho wa siku zikaharibika,kwa hiyo sisi kama walimu tumejifunza mengi na tutawaambia wenzetu kwamba rushwa ina atahari kubwa sana kwa taifa letu,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news