Klabu ya Liverpool inaweza kumpoteza mshambuliaji Mohamed Salah (28) kwenye michuano tofauti msimu ujao, kwa mujibu wa Mirror, Salah atakuwa na kibarua nchini Misri.Ni baada ya kocha wa nchi hiyo wa vijana wa chini ya miaka 23, kuthibitisha tena nia yake ya kumchukua kwa ajili ya michezo ya Olimpiki.
Wakati huo huo,Sky90 via Star inaripoti kuwa,mshambuliaji wa Borussia Dortumund Erling Braut Haaland (20) ameungwa mkono kujiunga na Liverpool badala ya Manchester United na Mkurugenzi wa michezo wa RB Salzburg, Christoph Freund. Nyota huyo alijiunga na Dortmund akitokea Salzburg mapema mwaka huu.
Kwa upande wa 90min, wamebainisha kuwa,winga wa Mexico na Cruz Azul Orbelin Pineda (24) anafuatiliwa na Arsenal, Tottenham, Wolves, Everton, Southampton, Newcastle na West Ham.
Huku Herfordshire Mercury ikiripoti kuwa,
Kocha wa Watford, Vladimir Ivic ameeleza masikitiko yake baada ya kushindwa kumsajili beki mpya wa kushoto. Kwa upande wa Football Insider,mmiliki wa klabu ya Tottenham, Joe Lewis ameruhusu mshambuliaji wa Korea Kusini, Song Heung-min (28) kupewa mkataba wenye thamani ya pauni 200,000 kwa wiki na marupurupu mengine.
Nao Manchester Evening News wanaeleza kuwa,Klabu ya Manchester United wametakiwa kuchangamka kwenye dirisha la usajili la mwezi Januari, 2021.