Tetesi:Chelsea inamfukuzia Jude Bellingham

Kwa mujibu wa Goal, mazungumzo ya mkataba wa Watford na Adama Traore (24) yamekwama kutokana na kile ambacho kinatwajwa kuwa, winga huyo hafurahii muda anaopewa kucheza. Hayo yanajiri ikwa awali Traore alihusishwa na taarifa za kuhamia klabu ya Barcelona.

Eurosport inaripoti kuwa, Klabu ya Chelsea inataka kusaini mkataba na kiungo wa Borussia Dortmund na England, Jude Bellingham (17) badala ya kiungo wa kati wa West Ham, Declan Rice (21).

Wakati hayo yakijiri, Klabu ya West Ham imepewa ofa ya kusaini kandarasi na mshambuliaji wa Real Mdrid ambaye ni raia wa Uhispania, Mariano Diaz (27).

Talksport wanadokeza kuwa, Klabu ya Arsenal inaangalia uwezekano wa kufanya mkataba wa kubadilishana wachezaji na Inter Milan ambao utamuwezesha Mdenmark na mlinzi wa zamani wa Tottenham, Christian Eriksen (28) kujiunga nao na kiungo wa kati Mswiss, Granit Xhaka (28) kuhamia katika klabu hiyo ya Italia.

Pia Evening Standard imedai kuwa, klabu ya Arsenal ipo katika mazungumzo ya kumuuza beki Mfaransa, William Saliba kwa mkopo msimu ujao.

Aidha, Mirror inaripoti kuwa, kiungo wa kati wa zamani wa Juventus, Midfielder Claudio Marchiso amemtaka mchezaji wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba (27) arejee katika klabu hiyo ya Italia.

Kwa mujibu wa Sun, mshambuliaji wa zamani wa Manchester City na Liverpool, Mario Balotelli (30) amefanya mazungumzo na timu ya Championi ya Barnsley, kwani yuko huru baada ya mkataba wake na Bresica kusitishwa kwa kutohudhuria katika mazoezi.

Mail inatujuza kuwa, Klabu ya Leicester inamfuatilia kwa karibu kiungo wa safu ya nyuma-kushoto, Mreno Nuno Mendes (18) ambaye anakipengele cha kumnunua cha pauni milioni 40 katika mkataba wake na Sporting Lisbon.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news