Timu ya wanawake Tanzania yawachapa Afrika Kusini 6-1

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake chini ya miaka 17 Novemba 8 imeibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Wanawake ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa mashindano ya Cosafa.

Huo ni mchezo wa tatu wa Tanzania ambapo mchezo wa kwanza ilishinda mabao 5-1 dhidi ya Comoro kisha ikachapwa mabao 2-1 dhidi ya Zimbabwe na hii imeibuka na ushindi huo mbele ya Afrika Kusini.

Aisha Masaka wa Tanzania ameibuka kuwa nyota wa mchezo baada ya kufunga mabao matano kwenye mchezo mmoja huku akiondoka na mpira.

Mwanadada huyo alipachika mabao hayo dakika ya 21,23,39,44 na 89 na lile moja la mwanzo kabisa lilifungwa na Mwamvua Haruna dakika ya 18. Aidha, bao pekee la kufuta machozi kwa Afrika Kusini limefungwa na Noela Luhala ambaye alijifunga dakika ya 79 Uwanja wa Oval nchini humo.
Kandanda safi likipigwa na mabinti hao katika Uwanja wa Oval Novemba 8,2020.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news