Trump adai kushinda, Biden aanza taratibu za utumishi

Mgombea Urais wa Chama cha Republican nchini Marekani, Rais Donald Trump amesema kuwa, ameshinda urais kwa kura halali milioni 71,000,00, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Trump ambaye ni Rais anayemaliza muda wake baada ya Uchaguzi Mkuu wa Novemba 3, 2020 amesema, ushindi huo ni mkubwa zaidi dhidi ya mpinzani wake Rais mteule wa Marekani, Joe Biden.
"Waangalizi hawakuruhusiwa katika vyumba vya kuhesabia kura, nimeshinda uchaguzi, nimepata kura halali milioni 71,000,000. Jambo baya limejitokeza pale ambapo waangalizi wetu hawakuruhusiwa kuona, hayakutokea awali, mamilioni ya barua yalitumwa kwa watu ambao hawakustahili,"amelalama Donald Trump kupitia ukuta wake wa Facebook.

Wakati Donald Trump akidai hayo, Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden ambaye kwa sasa ni Rais mteule wa Marekani amesema kuwa,atakuwa Rais ambaye ni kiunganishi na si kuwagawa Wamarekani.

Joe Biden ameyasema hayo Novemba 7, 2020 katika hotuba yake ya kwanza kama Rais mteule wakati akiwahutubia maelfu ya wananchi kutoka mjini Wilmington, Delaware Marekani.

Akirejea hotuba zake za zamani, Biden amesema ni huu ni wakati wa kuepuka siasa za chuki, kupunguza jazba, kukutana tena, "na kusikilizana kati yetu,”amesema.

Joe Biden amewasihi wafuasi wake wawasiliane na wale ambao hawakumpigia kura, na amekiri kuna wenye masikitiko wale waliomuunga mkono Rais Donald Trump.

“Nimeshindwa mara kadhaa,sasa, kila mmoja ampe mwenzake fursa,"amesema Joe Biden Rais. Pia amesema kuwa Jumatatu atazindua kikosi kazi cha COVID-19 kilichojikita katika sayansi kuanza kazi ya kudhibiti janga hilo, ambalo takwimu za Chuo Kikuu cha Johns Hopkins zinaonyesha limeambukiza zaidi ya Wamarekani milioni 9.8 na kuua zaidi ya watu 237,000.

Akiwa anajulikana katika siasa za Washington kwa karibu nusu karne, Biden anatarajiwa kuapishwa Januari 20, pamoja na Makamu wa Rais Mteule Kamala Devi Harrism ambaye kwa sasa ni Seneta wa California.

Joe Biden alitambulishwa Jumamosi usiku na Harris, binti wa wahamiaji ambaye atakuwa mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi na mwenye asili ya India kuhudumu nafasi ya Makamu wa Rais nchini Marekani.

“Wakati demokrasia yetu ilipokuwa kwenye kura katika uchaguzi huu, na roho ya Marekani kuwa hatarini na Dunia ikiangalia, imeleta siku mpya kwa Marekani,”amesema Harris mbele ya mamilioni ya Wamarekani huku salamu za pongezi zikiendelea kumiminika kila kona ya Dunia.

Pia amewashukuru wapiga kura nchini kote kwa kujitokeza kwa idadi kubwa na kufikisha ujumbe uliowazi huku akisisitiza kuwa, wamechagua matumaini, umoja, heshima na sayansi, "na ndio, ukweli, mmemchagua Joe Biden kuwa rais ajaye wa Marekani,"amefafanua Kamala.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news