Ulaya yakubali kutoa dola milioni 116 kwa Msumbiji

Umoja wa Ulaya umekubali kutoa dola milioni 116 kwa Serikali ya Msumbiji kusaidia kupambana na janga la virusi vya Corona (COVID-19), anaripoti Mwandishi Diramakini.
Umoja huo ulipunguza msaada wake wa kifedha kwa Msumbiji mwaka 2016 baada ya nchi hiyo kufichua taarifa za kuwa na madeni mengi kutokana na mkopo, yaliyokuwa yamesimamiwa na Serikali.

Serikali ilikuwa imeficha taarifa kuhusu mikopo hiyo. Wafadhili wengine ikiwemo Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), walisitisha msaada wao kwa Msumbiji.

Balozi wa Umoja wa Ulaya, Antonio Sanchez-Benedito Gaspar amewaeleza waandishi wa habari mjini Maputo,Msumbiji kwamba msaada huo utatumika moja kwa moja kusaidia watu wa Msumbiji kukabiliana na athari za kiuchumi kutokana na janga la virusi hivyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news