Upelelezi kesi aliyekuwa Bosi MSD haujakamilika

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam,imesema kuwa upelelezi katika Kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na Kaimu Mkurugenzi wa Lojistiki, Byekwaso Tabura, bado haujakamilika.
Hayo yameelezwa leo Novemba 4,2020, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate na wakili wa Serikali Sophia Nyanda, na kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 19,mwaka huu. 

Miongoni mwa mashitaka yanayowakabili washtakiwa ni kati ya tarehe 1 Julai, 2016 na 30 Juni, 2019 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, kwa makusudi washtakiwa waliongoza genge la uhalifu. 

Shtaka la pili ni kuisababishia hasara MSD, tukio wanalodaiwa kulitenda kati ya Julai Mosi, 2016 na tarehe 30 Juni, 2019, katika eneo la MSD lililopo Keko, washtakiwa waliisababishia MSD hasara ya shilingi bilioni 3.8. 

Pia, Bwanakunu, anadaiwa kati ya tarehe 1 Julai, 2016 na 30 Juni, 2019 katika Ofisi za MSD zilizopo Keko, kwa makusudi alikiuka sheria ya umma kwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kuwaongezea nyongeza ya mishahara na posho wafanyakazi wa MSD, bila kibali cha Katibu Mkuu Utumishi na hivyo kuisababishia hasara mamlaka hiyo kiasi cha shilingi bilioni 3. 

Shtaka la nne ni kuisababishia hasara ya shilingi 85 milioni mamlaka, shtaka linalowakabili washtakiwa wote, huku katika shtaka lingine wakituhumiwa kutakatisha fedha kiasi cha shilingi bilioni 1.6. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news