Kikundi cha watu wachache chenye nia ovu kimebuni namna ya kuwatapeli Watanzania kupitia https://vodacomzawadi.com/tz/#1604491380566 kwa madai kuwa wao ni sehemu ya Kampuni za Simu za Mkononi Tanzania ya Vodacom, Mwandishi Diramakini amefichua.
"Zawadi za Vodacom, angalia ikiwa nambari yako imechaguliwa na Vodacom kupokea * TSH 87,500 * kama sehemu ya mpango wao wa kuzawadi wateja ambao wametumia Mpesa kwa zaidi ya miezi mitatu.Watumiaji wa Vodacom tu. Tarehe ya mwisho ni 2020-12-5," imesomeka sehemu ya ujumbe unaosambaa makundi mbalimbali ya Whatssap.
Uchunguzi wa awali uliofanywa na Mwandishi Diramakini umebaini kuwa,
kikundi hicho kinatumia ujumbe ambatanishi wa maneno ya yenye
kuwaaminisha wameshinda na wakishafungua kiambatanisho cha tovuti
wanaelekezwa kujaza majina yao kamili.
Aidha, baada ya kujaza majina, hatua inayofuata wahuni hao wanakuelekeza ili uweze kufikia lengo la kupata zawadi unapaswa kushirikisha ujumbe huo kwa makundi ya Whatsapp 12 kwa hatua inayofuata.
Mwandishi Diramakini amefuata hatua kwa hatua utaratibu huo ili kujiridhisha na hayo wanayosema, alichobaini ni kwamba kikundi hicho kimedhamiria kuwalaghai Watanzania. Hata hivyo, juhudi zinaendelea ili kupata taarifa za kina kutoka Vodacom Tanzania kuhusiana na uhusiano wao na kikundi hicho ambacho kinatumia vibaya jina la kampuni hiyo kwa ajili ya kuwalaghai wateja wao.

Taarifa kwa wateja wa Vodacom Tanzania. Ukipata ujumbe huu, tafadhali wafahamishe na wengine.
Tags
Habari
Nice
ReplyDeleteHONGERA SANA MWANDISHI DIRAMAKINI, HUU NDIYO UANDISHI TUNAOTAKA, MAANA KWA UJUMBE HUU TUNAWEZA KUTAPELIWA WENGI, UMETHUBUTU, TUNASUBIRIA TAARIFA KUTOKA HUKO VODAKOM ILI KUFAHAMU ZAIDI HATUA WANAZOCHUKUA KUTULINDA WATEJA WAO.
ReplyDelete