"Navishukuru sana vyombo vya ulinzi na usalama, kwa kuimarisha hali ya ulinzi na usalama tangu lilipoanza zoezi zima la Uchaguzi mpaka sasa limekamilika kwa mtu aliyeshinda anaapishwa.Asanteni sana vyombo vya ulinzi na usalama nawasihi Watanzania tuendelee kuitunza amani yetu,"amesema hayo leo Novemba 5,2020 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli baada ya kuapishwa jijini Dodoma.