Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limewataka wabunge wateule kutambua kuwa, kila mmoja anapaswa kuambatana na wageni wasiozidi 20 wakati wa zoezi la kuapa, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Zoezi la kuapa kwa wabunge hao wateule ambao walipatikana baada ya Uchaguzi Mkuu wa Novemba 28, mwaaka huu linatarajiwa kufanyika Novemba 10 hadi 12, 2020 bungeni jijini Dodoma.
Hayo yamebainishwa leo Novemba 8, 2020 na Katibu wa Bunge, ndugu Stephen Kagaigai kupitia taarifa aliyoitoa kwa umma.

Pia Katibu huyo wa Bunge amesema kuwa, zoezi la kuapa litafanyika kwa haraka na kwa muda mfupi kwa kuzingatia ratiba ya mkutano. "Hivyo, wabunge wateule tunawaomba kuzingatia tangazo hili,"ameeleza Katibu huyo.
Tags
Habari