Wafanyabiashara wa vileo Zanzibar watakiwa kukamilisha taratibu

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

BODI ya Ushauri na Udhibiti wa Vileo Zanzibar imewataka wafanyabishara wa vileo kuhakikisha wanakamilisha taratibu za maombi ili kufanyiwa ukaguzi na kupatiwa leseni.

Mwenyekiti wa bodi hiyo, Abdulrazak Abdulkadir Ali ameyabainisha hayo baada ya kufanya ukaguzi kwenye maeneo ya wafanyabiashara na wasambazaji wa vileo ambao wamekamilisha taratibu jijini Zanzibar.

Ali amesema, lengo la ukaguzi huo ni kutekeleza sheria mpya ya vileo, Sheria Namba 9 ya mwaka 2020 ambayo ina lengo la kudhibiti utitiri wa baa zisizo na leseni na ambazo zinaendeshwa kinyume na sheria nchini.

Pia Mwenyekiti huyo amesema, sheria hiyo imekuja na mabadiliko makubwa hasa baa zilizokaribu na makazi ya watu ambazo amesema zimepungua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

2 Comments

  1. Marekebisho kidogo tafadhali: Ni Sheria Namba 9 ya mwaka 2020 na sio sheria namba 7

    ReplyDelete
  2. Asante sana ndugu kwa masahihisho.

    Nasi tutarekebisha

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news