Wairan wahukumiwa miaka 30 jela kwa kukamatwa na heroin Tanzania

Mahakamu Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imewatia hatiani na kuwahukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 watuhumiwa wawili raia wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Raia hao ni nahodha Nabibaksh Pribaksh Bidade na Mhandisi Muhamad Hanif wa jahazi lililohusika kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa kilo 111.02, kilo 3.34 za bangi na gramu 235.78 za bangi iliyosindikwa.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Florence Khambi, pia Mahakama imewaachia huru watuhumiwa wengine 11 na kutaifisha jahazi lililohusika kusafirisha dawa hizo na imeamuru dawa husika ziteketezwe.

Washtakiwa walioachiwa huru ni Abdallah Sahib, UIbeidulla Abdi, Naim Ishaqa, Moslem Golmohamad, Rashid Badfar, Omary Ayoub, Tahir Mubarak and Abdulmajid Pirmuhamad, ambao wote ni raia wa Iran pamoja na watanzania wawili, Ally Abdallah na Juma Amour.

Hukumu ya kesi hiyo ya uhujumu uchumi Namba 14/2018 ya Jamhuri dhidi ya Nabikash Pribakish Bidade na wenzake 12 imesomwa na Jaji Imakulata banzi wa Mahakamau Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Novemba 6,2020.

Mawakili wa Serikali, Monica Mbogo na Cecilia Shelli wamesimama upande wa Serikali na Mawakili wa Utetezi walikuwa ni Juma Nassoro na Jethro Tiliemwesiga.Nabibaksh Pribakish Bibade na wenzake 12 walikamatwa Oktoba 24, 2017 majira ya saa nne na robo usiku katika Bahari ya Hindi na maafisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya wakishirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ambapo kesi husika ilijumuisha raia 10 wa Iran na Watanzania watatu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news