Wakili wa Kenya, Paul Gicheru amejisalimisha kwa viongozi wa Uholanzi ili kukabiliana na mashtaka dhidi yake kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), anaripoti Mwandishi Diramakini.
Wakili huyo anadaiwa kuwahonga mashahidi katika kesi dhidi ya Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto katika mahakama hiyo.Wakili
Gicheru alikuwa anatafutwa na warranti ya ICC tangu mwaka wa 2015,
akituhumiwa kujaribu kuwapa hongo mashahidi sita wa muendesha mashtaka
ili wabadili ushahidi wao katika kesi dhidi ya Ruto.
Ruto
na mwanahabari Joshua Sang, walishtakiwa kwa kuchochea ghasia za
kikabila baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata wa mwaka 2007 ambapo watu
1,200 waliuwawa.
Mwaka
2016, majaji waliamuru kwamba hakuna kesi yoyote ya kufuatilia, licha
ya kuwa walitoa nafasi ya kupokea mashtaka mapya, wakihisi kwamba kesi
hiyo ilidhoofishwa na muingilio wa siasa na vitisho dhidi ya mashahidi.
Kwa
mujibu wa Reuters, msemaji wa Ruto hakupendelea kutoa maelezo yoyote
kuhusu kesi ya Wakili Gicheru, lakini alisisitiza kwamba,Wakili Gicheru
hakuwahi kufanya kazi kama wakili wa Ruto.