Wanawake watoa ya moyoni Jukwaa la Women Health Talk

Wanawake wanakabiliwa na changamoto nyingi ambazo hawana majibu yake, wengine hawajui wapi wanakoweza kupata ufumbuzi, hali inayowasababishia baadhi yao kujikuta wakipata magonjwa mbalimbali na hata unyanyasaji wa kijinsi na kingono.

Mwanzilishi wa Jukwaa la Women Health Talk 2020 ambaye ni mtaalamu wa Afya ya Jamii kutoka Doctor’s Plaza Polyclinic, Sophia Byanaku akiwakaribisha washiriki wa jukwaa hilo ambao ni wanawake kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es Salaam wakati wa mkutano huo uliozungumzia jinsi ya kuweza kuyafahamu na kukabiliana na matatizo mbalimbali ya kiafya yanayowakabili wanawake.

Hayo yamebainishwa Novemba 5, 2020 wakati wa majadiliano kwenye Jukwaa la Women Health Talk 2020 lililowakutanisha wanawake wa taaluma mbalimbali pamoja na wataalamu mabingwa wa magonjwa ya binadamu ikiwamo ya kina mama, moyo, saratani na kisukari.

Prof. Sylivia Kaaya kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) akizungumzia kuhusu msongo wa mawazo na maisha ya mwanamke katika Dunia ya leo wakati wa Jukwaa la Women Health Talk 2020 lililofanyika jijini Dar es Salaam ambalo liliandaliwa na Doctor’s Plaza Polyclinic kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), GSM Tanzania, Hyatt Regency Hotel, MultiChoice Tanzania (DSTV), Ajanta Pharma na Masilamani KasMedics.

Akiwasilisha mada katika jukwaa hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Tanzania Health Promotion Support (THPS), Dkt.Redempta Mbatia amesema wapo baadhi ya wanawake waliowahi kujihusisha na biashara ya kuuza miili yao, lakini sasa wameacha na wanajuta kwamba walidhalilisha familia zao.

“Taasisi yetu inafanya kazi kwa karibu na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, tumeweza kukutana na wanawake 28,000 kati ya hao 20,000 walikuwa wakijiuza miili yao (wadada poa) na theluthi yao wana maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitoa mada kuhusu magonjwa ya moyo kwa wanawake wakati wa Jukwaa la Women Health Talk 2020 lililofanyika leo jijini Dar es Salaam lililoandaliwa na Doctor’s Plaza Polyclinic kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), GSM Tanzania, Hyatt Regency Hotel, MultiChoice Tanzania (DSTV), Ajanta Pharma na Masilamani KasMedics.
 
“Kwa kundi hili kiwango cha maambukizi ya Ukimwi ni kikubwa kuliko hata makundi mengine kwenye jamii na ile ni tabia hatarishi ambayo wanafanya inawaingiza kwenye maambukizi, lakini wengi wao wanaingia huko tuliowahoji walidai wanahitaji kujikwamua kiuchumi,”amesema.

Amesema, kupitia shirika hilo lilipata ufadhili na kuvifikia vikundi 250 vya ujasiriamali kwa kundi hilo na kila kimoja kina wasichana (young womens) 12.

Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbi (MNH) Blenda Balandya akizungumzia kuhusu matatizo la kiafya yanayosababisha watu kutokupata watoto wakati wa Jukwaa la Women Health Talk 2020 lililofanyika jijini Dar es Salaam ambalo liliandaliwa na Doctor’s Plaza Polyclinic kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), GSM Tanzania, Hyatt Regency Hotel, MultiChoice Tanzania (DSTV), Ajanta Pharma na Masilamani KasMedics.

“Waanzisha miradi wanafanya kazi, wengi wanajuta, wameacha sasa tabia hiyo na wengine wamekuwa madiwani katika uchaguzi wa hivi karibuni, mwaka huu, wapo wanaohuzunika kwamba wamejisikia vibaya sana kwani wamedhalilisha hata watoto wao.
 
“Wengine wamejuta wazi wazi kwenye mikutano kwa kujihusisha na biashara hiyo, wapo pia wa-kaka poa tunaowaona, unyanyapaa ni mkubwa na wengi wanajificha hasa vijana, walioko vyuoni, kuhusu ukimwi,” amebainisha.

Baadhi ya washiriki wa Jukwaa la Women Health Talk 2020 lililofanyika jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada ya ulaji wa chakula unaofaa na wanawake wakati wa Jukwaa la Women Health Talk 2020 ambalo lililoandaliwa na Doctor’s Plaza Polyclinic kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), GSM Tanzania, Hyatt Regency Hotel, MultiChoise Tanzania (DSTV), Ajanta Pharma na Masilamani KasMedics.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Sikudhani Muya ameshauri wanawake kujenga utamaduni wa kuchunguza afya zao mara kwa mara.

“Kwa sababu, kwa mfano magonjwa ya saratani yanapogundulika mapema ni rahisi kutibika na kupona,” ameshauri. Kwa upande wake, Prisca Liymo ambaye ni mshiriki wa mkutano huo amesema umefanyika wakati mwafaka na umewapa maarifa mapya.

Baadhi ya washiriki wa Jukwaa la Women Health Talk 2020 lililofanyika jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada ya ulaji wa chakula unaofaa na wanawake wakati wa Jukwaa la Women Health Talk 2020 ambalo lililoandaliwa na Doctor’s Plaza Polyclinic kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), GSM Tanzania, Hyatt Regency Hotel, MultiChoise Tanzania (DSTV), Ajanta Pharma na Masilamani KasMedics.

“Ni jukwaa zuri mno, litasaidia mno kundi la wanawake na sisi vijana mtukumbuke, naomba mtuandalie jukwaa kwa ajili yetu, tuna maswali lukuki hususan kuhusu afya ya uzazi.

“Pengine mimi ndiye mshiriki mwenye umri mdogo zaidi humu ndani, nilipopata mwaliko kuhudhuria mkutano huu nilifurahi mno, vijana tuna maswali mengi na hatuna majibu, naomba waandaaji wakati mwingine mtufikirie, mtuandalie la kwetu pia, tukutanishwe na wataalamu wa afya, tuulize,” ametoa ombi.

Miss Tanzania 2001 Happiness Magese akiuliza swali wakati wa Jukwaa la Women Health Talk 2020 lililofanyika jijini Dar es Salaam lililoandaliwa na Doctor’s Plaza Polyclinic kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), GSM Tanzania, Hyatt Regency Hotel, MultiChoise Tanzania (DSTV), Ajanta Pharma na Masilamani KasMedics.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwanzilishi wa jukwaa hilo, lililo chini ya Doctors Plaza Polyclinic, Sophia Byanaku, amesema “Mimi si daktari kitaaluma, lakini shughuli zangu nafanya katika mazingira ya hospitali pale Doctors Plaza Polyclinic, ni ‘Public Health Specialist’, nimesoma shahada yangu ya pili pale chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na nchini Norway kwa hiyo muda mwingi huwa nipo hospitalini.

Dkt. Jessie Mbwambo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akiwashauri wanawake waliohudhuria Jukwaa la Women Health Talk 2020 ambalo liliandaliwa na Doctor’s Plaza Polyclinic kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), GSM Tanzania, Hyatt Regency Hotel, MultiChoise Tanzania (DSTV), Ajanta Pharma na Masilamani KasMedics kuwauliza madaktari ni dawa aina gani wanazowapatia pamoja na kazi zinazofanya mwilini kabla ya kuanza kuzitumia pindi wanapouugua.

“Nimegundua kwamba wanawake tunapitia changamoto nyingi na hatuna majibu ya changamoto hizo, nikaona vema nianzishe jukwaa hili kuwakutanisha wanawake na wataalamu wa afya ili kwa pamoja tuzungumze ili kuweza kupata ufumbuzi katika yale tunayoyapitia,” amesema.

Dkt. Sikudhani Muya kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) akitoa mada kuhusu saratani zinazowapata wanawake wakati wa Jukwaa la Women Health Talk 2020 lililofanyika jijini Dar es Salaam ambalo liliandaliwa na Doctor’s Plaza Polyclinic kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), GSM Tanzania, Hyatt Regency Hotel, MultiChoise Tanzania (DSTV), Ajanta Pharma na Masilamani KasMedics.

Amesema, anakusudia jukwaa hilo kuwa endelevu katika miaka ijayo ili liweze kufikia kundi kubwa zaidi la wanawake na vijana wanufaike na elimu ya afya kutoka kwa wataalamu mabingwa.

Jukwaa hilo la kwanza lililohudhuriwa na washiriki 192 limeandaliwa na Doctor’s Plaza Polyclinic kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), GSM Tanzania, Hyatt Regency Hotel, MultiChoise Tanzania (DSTV), Ajanta Pharma na Masilamani KasMedics.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news