Wenye ulemavu wa macho watoa ombi elimu ya afya

Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Macho (TLB) mkoani Iringa kimeeleza kuwapo kwa hofu juu ya wanachama wake kuambukizwa magonjwa ya milipuko kutokana na kundi hilo kutopatiwa elimu ya kujikinga magonjwa hayo, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mwenyekiti wa TLB mkoani Iringa, Huruma Maketa amesema, tangu kuibuka kwa maambukizi ya virusi vya Corona nchini kundi la walemavu walikuwa wanahitaji elimu maalum kwa ajili ya kuhakikisha wanajikinga na ugonjwa huo kwa kuwa kundi hilo halijawahi kukumbukwa na walikuwa hatarini zaidi kupata maambukizi hayo.

Maketa amesema kuwa, kundi hilo limekuwa likisahaulika mara kwa mara kupata elimu ya magonjwa ya milipuko kuliko makundi mengine yote hivyo serikali na wadau wengine wanapaswa kujitolea kutoa elimu kwa walemavu hao.

Amesema kuwa, kunapotokea milipuko ya magonjwa kama kipindupindu,homa ya matumbo na Corana wanakuwa hawapata elimu hiyo kwa wakati na kushindwa kupata mbinu sahihi za kujikinga na magonjwa hayo.
Mwenyekiti wa TLB Manispaa ya Iringa, David Mgimwa akizungumza na waandishi wa habari juu la ombi lao la kupewa elimu ya magonjwa ya milipuko.

Maketa amesema kuwa, watu wenye ulemavu hawaoni mambo yanayoendelea kutokana wao kuweza kusikia tu, hivyo ikitolewa elimu mara kwa mara itasaidia kundi hilo kuepukana kukumbwa na magonjwa hayo ya milipuko.

Aidha, kwa upande wake Mwenyekiti TLB Manispaa ya Iringa, David Mgimwa amesema kuwa, walikuwa wanakukumbana na unyanyapaa kutoka kwa watu waliokuwa wakiwasaidia kuwaongoza barabarani kukataa kuwashika mkono wakati wa kipindi cha Corona kwa hofu ya kupata maambukizi hayo.

Mgimwa amesema kuwa, wananchi wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa watu wenye ulemavu ili kuwasaidia kuepukana na kujikinga na magonjwa ya milipuko ambayo yanayokuwa yanatokea mara kwa mara bila watu wenye ulemavu kujua nini kinaendelea wala kutokujua namna ya kujikinga na magonjwa hayo.

Mgimwa amewaomba wananchi kuendelea kuwasaidia na kutoa elimu kwa watu wenye ulemavu wa macho pale yanapotokea magonjwa ya milipuko ili kuwasaidia walemavu hao kujikinga kupata magonjwa hayo ya milipuko.

Lakini pia jamii imeshauriwa kuwashika mkono watu wenye ulemavu wa macho hasa katika kipindi cha mapambano dhidi ya kuenea kwa virusi vya Corona COVID 19 kwani wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali kutokana na hali zao.
 
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Iringa, Dkt.Jesca Leba amesema kwamba, kutokana na hali walizonazo walemavu wa macho kuna umuhimu mkubwa wa jamii kuwa nao sambamba kwani wako katika hali ya hatari zaidi kutokana na hali zao za kutokuona hivyo elimu na kuwaongoza namna ya kunawa mikono itasaidia katika mapambano hayo.

Amesema kuwa, kama manispaa wametoa mafunzo kwa walemavu na wataendelea kutoa mafunzo kwa makundi mbalimbali ya walemavu kwa ajili ya kushikwa mkono kwani changamoto kubwa kwenye vyombo vya kunawia mikono wanashindwa kuelewa mahali ilipo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news