Shirika la Umoja wa Mataifa linaloangazia masuala ya Afya Duniani (WHO) limezishauri nchi za Afrika kuandaa mipango ya kusambaza chanjo za kukabiliana na virusi vya Corona (COVID-19) kadri zitakavyopatikana, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Hayo yamebainishwa na Dkt.Matshidiso Moeti ambaye ni Mkurugenzi wa Kanda wa WHO wa Afrika kupitia taarifa yake iliyonukuliwa katika vyombo mbalimbali vya habari.
Kwa mujibu wa utafiti mpya wa WHO, nchi nyingi za Afrika haziko tayari kwa kile kitakachokuwa harakati kubwa zaidi ya chanjo barani humo dhidi ya virusi hivyo.
"Tunapaswa kupanga na kuandaa mikakati kutafanikisha au kuharibu shughuli hii ambayo haijawahi kutokea na tunahitaji uongozi na ushiriki kutoka ngazi za juu za serikali na mipango thabiti, ya kina ya uratibu wa kitaifa na mifumo iliyowekwa,"amesema.
Kwa sasa wataalam na kampuni mbalimbali duniani zinaendelea na mchakato wa mwisho wa kukamilisha upatikanaji wa chanjo dhidi ya virusi vya Corona ambavyo vimesababisha vifo vya maelfu ya watu duniani kwa sasa.