Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imewatangaza wajumbe 18 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi za Viti Maalum vya Wanawake vya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, anaripoti Jaala Makame Haji (ZEC).
Tume imetangaza majina ya wajumbe hao katika mkutano wake uliofanyika leo Novemba 7, 2020 katika ukumbi wa mikutano wa tume hiyo uliopo Maisara jijini Zanzibar.
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imewatangaza wajumbe 18 kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa mujibu wa masharti na maelekezo ya Ibara ya 67 ya Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984.
Aidha, tume imewatangaza wajumbe hao baada ya kuridhika kuwa wote wana sifa ya kuwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kama zilivyoainisha katika Katiba ya Zanzibar Ibara ya 68.
Waliotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar ni;
1. Bi.Panya Ali Abdallah
2. Bi. Bihindi Hamad Hassan
3. Bi.Salma Mussa Bilal
4. Bi.Shadya Mohammed Suleiman
5. Bi.Fatma Ramadhan Mohamed (Mandoba)
6. Bi.Saada Ramadhan Mwenda
7. Bi.Mwantatu Mbaraka Khamis
8. Bi.Zainab Abdalla Salum
9. Bi.Riziki Pemba Juma
10. Bi.Leila Mohamed Mussa
11. Bi.Salha Mwinyi Juma
12. Bi.Hudhaima Mbarak Tahir
13. Bi.Sabiha Fil fil Thani
14. Bi.Aza Januar Joseph
15. Bi.Mwanaid Kassim Mussa
16. Bi.Mgeni Hassan Juma
17. Bi.Mwanajuma Kassim Makame
18. Bi.Rahma Kassim Ali.
Hata hivyo, tume tayari imeshawasilisha majina ya Wajumbe hao kwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria.
Tags
Zanzibar