Meneja wa Benki ya Akiba Commercial Plc (ACB) tawi la Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Joachim Mowo (kushoto) akizungumza na wanachama wa Taasisi ya FATA Vicoba Endelevu wakati wa hafla ya mkutano wao wa mwisho wa mwaka wa taasisi hiyo, mkutano huo umedhaminiwa na Benki ya ACB kwa lengo la kukuza na kunufaisha wajasiriamali wadogo na wakubwa.
Hafla hiyo imefanyika Desemba 19, 2020 katika ukumbi wa 361 uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam (wa pili kushoto) ni Mwenyekiti wa Taasisi FATA Vicoba Endelevu, Hanipha Tarimo, Katibu wa taasisi hiyo, Rehema Sombi pamoja na Mtunza Fedha, Jefferson Makubo. Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Mwanasheria Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Godfrey Songolo.
Baadhi ya wanachama wa Taasisi ya FATA Vicoba Endelevu na wateja wa Benki ya ACB wakiwa katika hafla ya mkutano wao wa mwisho wa mwaka uliodhaminiwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Godfrey Songolo ambae pia alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya mkutano wao wa mwisho wa mwaka wa Taasisi ya FATA Vicoba Endelevu, mkutano umedhaminiwa na Benki ya ACB kwa lengo la kukuza na kunufaisha wajasiriamali wadogo na wakubwa ili waweze kutimiza ndoto zao kupitia benki hiyo. Hafla hiyo imefanyika Desemba 19, 2020 katika ukumbi wa 361 uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi FATA Vicoba Endelevu, Hanipha Tarimo akitoa ufafanuzi kuhusu taasisi hiyo wakati wa hafla ya mkutano wao wa mwisho wa mwaka wa taasisi hiyo ambapo mkutano huo umeodhaminiwa na Benki ya ACB kwa lengo la kukuza na kunufaisha wajasiriamali wadogo na wakubwa ili watimize ndoto zao kupitia Benki ya ACB.
Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa 361 uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Kinondoni Kata ya Mwananyamala, Mulinga Samangwa, Meneja wa Benki ya Akiba Commercial Plc (ACB),Tawi la Kijitonyama, Joachim Mowo, Katibu wa Taasisi ya FATA Vicoba Endelevu, Rehema Sombi, pamoja na Mtunza fedha wa taasisi hiyo Jefferson Makubo. Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Mwanasheria Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Godfrey Songolo
Meneja Masoko wa Benki ya Akiba Commercial Plc (ACB), Innocent Ishengoma akizungumza na wanachama wa Taasisi ya FATA Vicoba Endelevu wakati wa hafla ya mkutano wao wa mwisho wa mwaka wa taasisi hiyo ambapo mkutano huo umedhaminiwa na Benki ya ACB kwa lengo la kukuza na kunufaisha wajasiriamali wadogo na wakubwa ili watimize ndoto zao kupitia Benki ya ACB.
Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa 361 uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam. Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Mwanasheria Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Godfrey Songolo.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka Benki ya Akiba Commercial Plc wakiwemo viongozi na wanachama wa Taasisi ya FATA Vicoba Endelevu. (Picha zote na Mwandishi Diramakini.