ATCL: Safari za ndege Geita rasmi Januari 2021

Mkurugenzi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladslaus Matindi ametangaza kuwa Januari 9,2021 wataanza rasmi safari za ndege kutoka uwanja wa ndege mpya wa Geita uliopo wilayani Chato kwa safari za kwenda Mwanza hadi Dar es Salaam,anaripoti Robert Kalokola (Diramakini) Geita.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel, Mkurugenzi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladslaus Matindi na viongozi wengine wakiwa katika jengo la abiria katika uwanja wa ndege Geita uliopo wilayani Chato. (Picha Robert Kalokola/ Diramakini).

Amesema, uwanja huo uko kibiashara zaidi kutokana na kazi za kiuchumi zinazofanyika katika mkoa huo wa Geita.

Amesema kuwa, safari za ndege zitaanzia kutoka Chato kwenda Mwanza na kurudi Dar es Salaam na nauli itakuwa sh.239,000 kwenda tu na kwenda na kurudi ni sh.340,000.

Amesema safari hizo za ndege zitakuwa mara tatu kwa wiki ambazo ni siku ya Jumatatu, Alhamisi na Jumamosi.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel amesema mahitaji ya usafiri wa anga katika mkoa huo ni mkubwa hivyo ujio wa Shirika la Ndege katika uwanja huo imekata kiu katika mkoa huo.

Amekaribisha mashirika mengine kuleta ndege zake katika uwanja huo ili kupanua huduma na kuimarisha ushindani.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema kuwa, Wilaya ya Chato ina watu wengi ambao walikuwa wanahitaji kutumia uwanja huo wa ndege na walikuwa wanapata usumbufu kwenda mikoa ya jirani.

Amesema kuwa, uwanja huo utadumisha mahusiano ya mikoa na mikoa, lakini nchi na nchi jirani. Ameongeza kuwa, Geita wanahitaji kusafirisha mizigo kama vile samaki kwa sababu ni mkoa huo ni wavuvi wa samaki .

Hivi karibu Mamlaka ya Usafiri wa Anga,Shirika la Ndege pamoja na mamlaka ya usimamizi wa viwanja vya ndege nchini walifanya kikao cha pamoja wilaya kwa ajili ya kujiridhisha na utayari wa kuanza kutumika kwa uwanja huo .

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news