Wanalambalamba, timu ya Azam FC imemuuza mshambuliaji wake wake, Alain Thierry Akono Akono kwenda klabu ya Negeri Sembilan ya Malaysia, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Alain alijiunga na Azam FC mwanzoni mwa msimu huu akitokea klabu ya AS Fortuna ya Cameroon kwa mkataba wa miaka miwili.
Pia mpaka Azam FC inamuuza Akono mshambuliaji huyo amekuwa akikosa nafasi ya kuanza moja kwa moja katika kikosi hicho huku pia akiondoka akiwa hana bao katika Ligi Kuu Bara zaidi ya kufunga mara moja katika moja ya michezo ya kirafiki ya timu hiyo.
"Nikweli tumemuuza Alan Akono ambaye sasa anakwenda kuitumikia klabu ya Negeri Sembilan baada ya pande mbili kufikia makubaliano," amethibitisha Mkuu wa Idara ya Habari ya Azam FC Thabit Zakaria (Zaka Zakazi).
Kwa mujibu Azam FC imesema kwamba, wamefanikiwa kumuuza mchezaji huyo baada ya nusu msimu wa kuwa naye.
Akono anakuwa mchezaji wa tatu kuuzwa na Azam FC msimu huu baada ya kiungo Novatus Dissmas aliyejiunga na Maccabi Tel-Aviv ya Israel na mshambuliaji Shaaban Idd Chilunda aliyejiunga na Moghreb Atletic Tetouan Morocco ya Morocco.
Hata hivyo, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Azam FC, Thabit Zakaria amesema klabu itafanya usajili kabla ya dirisha dogo kufungwa.
Kwani, kuondoka kwa Akono kunampa fursa kocha, George Lwandamina kutafuta mbadala wake wakati huu akisubiri kurejea kwa mshambuliaji wao anayeongoza kwa ufungaji ndani ya timu hiyo, Prince Dube anayesubiri kupona mkono wake baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini.
Tags
Michezo