Azam FC yatoshana nguvu na Namungo FC

Wanalambalamba, Azam Fc ambao leo Desemba 14, 2020 walikuwa wenyeji wa Namungo FC kutoka mkoani Lindi wametoshana nguvu na kuibuka kwa matokeo ya 2-2, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mtanange huo umepigwa katika dimba la Azam Complex lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke katika Kata ya Chamanzi jijini Dar es Salaam.

Iddi Suleiman ndiye aliyewanyanyua mashabiki wa Wanalambalamba hao ndani ya dakika ya 19 na 74 ingawa mambo yalikwenda mrama baada ya Namungo FC kuyasawazisha kupitia Edward Charles Manyama dakika ya 25 na Stephen Sey dakika ya 90.

Leo inakuwa ni mechi ya tatu kwa Azam FC kukutana na Namungo FC ambayo imepanda Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/20.

Msimu uliopita mchezo wa kwanza Azam FC ilishinda kwa mabao 2-1 na mchezo wa marudio Namungo FC ilishinda bao 1-0 katika Uwanja wa Majaliwa, Lindi. 

Kwa matokeo hayo, Azam FC inafikisha alama 26 baada ya kucheza mechi 15 na inabaki nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye alama 29 za mechi 13 na Yanga SC wenye alama 37 za mechi 15 hadi sasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news