Bao la Rafael Leao sekunde ya 6 lavunja rekodi Serie A, Ligi Kuu Uingereza

Sekunde sita zimetosha kuifanya Klabu ya AC Milan kuingia katika historia mpya kupitia Ligi Kuu ya Italia ya Serie A baada ya fowadi matata, Rafael Leao (21) kuipachika bao Sassuolo, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mtanange huo wa aina yake umepigwa katika dimba la Mapei Stadium mjini Reggia Emilia, Italia ambapo bao la pili limefungwa na Mbeligiji Alexis Saelemaekers dakika ya 26. 

Hadi dakika 45 zinamalizika katika mtanange huo wa Desemba 20, 2020, AC Milan walikuwa wanaongoza kwa mabao mawili. 

Aidha, kipindi cha pili dakika ya 89,Domenico Berardi amewafuta machozi Sassuolo kwa bao moja. Hadi dakika ya mwisho, AC Milan wameibuka na alama tatu huku wakijivunia bao pekee la sekunde ya sita ambalo limewaweka katika rekodi ya kipekee.

Kwa matokeo hayo, AC Milan kwa sasa wapo kileleni kwa alama 31 katika msimamo wa Ligi hiyo wakifuatiwa na Inter Milan.

Wachambuzi wa soka wamemueleza Mwandishi Diramakini kuwa, bao la Leao limevunja rekodi ya Piacenzo Paolo Poggi aliyewahi kufungia AC Milan dhidi ya Fiorentina baada ya ya sekunde 8.9 za ufunguzi wa kipindi cha kwanza Desemba 2 mwaka 2001. 

Aidha, goli la Leao lilikuwa la haraka zaidi kuliko hata linaloshikilia rekodi katika soka ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) na ambalo lilifungwa na Shane Long wa Southampton dhidi ya Watford baada ya sekunde 7.69 pekee Aprili 23 mwaka 2019.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news