Beki wa zamani wa Manchester United, Gabriel Heinze (42) ameteuliwa kuwa kocha wa timu Atlanta inayoshiriki michuano ya Major League Soccer (MLS) huko Amerika, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Picha na Jam Media/Getty Images.
Kwa mujibu wa taarifa za awali beki huyo wa zamani amepewa kandarasi ya miaka miwili kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho. Anachukua nafasi ya kiungo wa zamani wa Aberdeen, Stephen Glass ambaye ndiye alikuwa kocha msaidizi wa kikosi cha Atlanta baada ya kuondoka kwa Frank de Boer Julai mwaka huu.
Heinze ambaye ni raia wa Argentina aliwahi pia aliwahi kuichezea Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa ikiwemo Real Madrid ya Uhispania.
Pia nyota huyo aliwahi kuchukua mikoba ya kikosi cha Velez Sarsfield kwa kipindi cha misimu miwili kabla ya 2019-20 kabla ya kuachana nao.
Tags
Michezo