Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Bia Africa Mashariki (EABL) leo Desemba 10,2020 imemtangaza Jane Karuku kuwa mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo inayomiliki Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Kampuni ya Bia ya Uganda (UBL) pamoja na Kampuni ya Bia ya Kenya (KBL).Jane Karuku, Mkurugenzi Mtendaji mpya EABL.
Jane Karuku ambaye alikuwa ni Mjumbe wa Nodi ya EABL na Mkurugenzi Mtendaji wa KBL, anachukua nafasi ya Andrew Cowan ambaye amekuwa mkurugenzi mtendaji wa EABL kwa miaka minne na nusu.
Cowan anakwenda kuchukua nafasi katika kampuni mama ya Diageo akiwa kama mkurugenzi mtendaji wa masoko ya Afrika.
Karuku ni kiongozi mahiri wa biashara mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 25. Kabla ya kujiunga na KBL, alikuwa ni rais wa asasi ya kimataifa isiyo ya kiserikali inayojulikana kama Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA) inayohusika na kuratibu ruzuku kutoka kwa mashirika makubwa yanayotoa ruzuku kwenye eneo la usalama wa chakula na maendeleo ya kilimo.
Pia amefanya kazi katika nyadhifa mbalimbali kwenye mashirika tofauti tofauti ikiwemo Cadbury’s East & Central Africa ambapo alikuwa ni mkurugenzi mtendaji ikiwa ni kabla ya kujiunga na Telkom Kenya kama naibu afisa mtendaji mkuu na katibu mkuu. Akiwa Cadbury alikuwa akihusika na nchi 14 zilizopo Afrika.
Pia amefanya kazi katika bodi mbalimbali kama Barclays Kenya na kwa sasa ni mjumbe wa shirika la Precious Sisters linalowasaidia wasichana wenye vipaji na wanaotoka katika mazingira magumu kupata elimu.
Kwa sasa pia ni mwenyekiti wa mpango wa Kenya Vision 20230 na pia aliongoza bodi ya kupambana na Covid-19 iliyoundwa na Rais Uhuru Kenyata wa Kenya.
John Musunga, Mkurugenzi mpya KBL.
Nafasi yake itachukuliwa na John Musunga ambaye atakuwa mkurugenzi mtendaji mpya wa KBL. Musunga ana uzoefu wa zaidi ya miaka 25 kwenye utawala, mauzo na masoko. Anajiunga na EABL kutoka GlaxoSmithKline (GSK).
Musunga amefanya kazi katika bodi mbalimbali na kwa nyadhifa tofauti tofauti. Amefanya kazi kama mjumbe wa bodi ya Kenya Vision 2030, mwenyekiti wa Kenya Association of Pharmaceuticals Industry na pia amefanya kazi kama mwenyekiti wa baraza la kibishara la HIV/AIDS.
Uteuzi wa Karuku na Cowan unaanza tarehe moja Januari 1, 2021 wakati wa Musunga utaanza rasmi tarehe 1 Machi 2021. Cowan ataendelea kuwa mjumbe wa bodi ya EABL