Fatou Bensouda ambaye ni Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya kushughulikia kesi za Jinai (ICC) ameitaka Serikali ya Sudan kutekeleza wajibu wake kivitendo katika suala la kutafuta haki kwenye jimbo la Darfur nchini humo, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Bensouda ameitaka serikali ya Sudan kuonesha kwa vitendo uwajibikaji wake katika suala la haki kwa watu wa jimbo la Darfur, kwa kuanza na hatua ya kuwaruhusu bila ya vipigamizi,wachunguzi wa mahakama hiyo kuwafikia mashahidi, maeneo ulikofanyika uhalifu pamoja na ushahidi mwingine katika eneo hilo la Magharibi.
Hayo ameyasema katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia maelezo aliyoyatoa kwa njia ya video ikiwa ni juhudi za kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19).
Bensouda amesema kwamba, hatilii shaka uaminifu wa maafisa wa ngazi za juu kutoka serikali ya mpito ya Sudan, lakini anasisitiza kwamba suala la wachunguzi kuruhusiwa kuingia Darfur ndilo hasa wanalolitarajia wahanga na ndicho kitu ambacho Sudan kwa uungaji mkono wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inachopaswa kukisimamia kwa sasa.

Tags
Kimataifa