Kocha wa zamani wa Klabu ya Liverpool, Gerard Houllier (73) amefariki, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Anakumbukwa zaidi kwa kuiwezesha klabu hiyo kutwaa vikombe sita ikiwemo FA Cup, UEFA Cup na League Cup kati ya 2000/01, ikifuatiwa na UEFA Super Cup na Charity Shield mwaka 2001 na League Cup mwaka 2003.
Kabla ya kifo chake aliweka wazi kuwa, atapambana ili kurejea katika hali ya kawaida kiafya.
Houllier ambaye pia amewahi kuifundisha Klabu ya PSG, Aston Villa na Lyon alifanyiwa upasuaji hivi karibuni.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Ufaransa,mzee huyo ambaye ni raia wa Ufaransa huenda amefariki kutokana na tatizo la shinikizo la damu ambalo lilikuwa linamkabili muda mrefu.
Vilabu viwili vya Ufaransa ikiwemo PSG na Lens ambavyo Houllier aliviongoza vimethibitisha kifo hicho.
Alikuwa Liverpool kuanzia 1998 na 2004, alifariki usiku wa kuamkia leo wakati akifanyiwa upasuaji wa moyo.
Tags
Michezo