Lewandowski awaangusha Messi, Ronaldo tuzo za FIFA

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetoa tuzo zake katika kutambua thamani ya kila mchezaji na kuongeza ushindani katika soka duniani, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Hata hivyo, baada ya baada ya kutaja tuzo mbalimbali FIFA ilitangaza pia kikosi cha msimu katika mashindano yote.

Katika kikosi ambacho kimetangazwa mjini Zurich, Uswisi mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo na wa FC Barcelona Lionel Messi wamefanikiwa kuingia ikiwa ni mara nyingi zaidi tangu mwaka 2007, hatua ambayo inatajwa kuwa nyota zao bado zinang'aa.

Pia mlinda mlango wa Liverpool, Allison Becker licha ya kukosa nafasi ya kutwaa tuzo ya kipa bora bado ametajwa kwenye kikosi hicho.

Majina hayo ya kikosi ni kama mlinda mlango, Alisson (Liverpool) wakiwemo walinzi Trent Alexander-Arnold (Liverpool), Virgil van Dijk (Liverpool), Sergio Ramos (Real Madrid), Alphonso Davies (Bayern Munich).

Wengine ni viungo akiwemo Joshua Kimmich (Bayern Munich), Kevin de Bruyne (Manchester City), Thiago (Liverpool) na fowadi Lionel Messi (Barcelona), Robert Lewandowski (Bayern Munich), Cristiano Ronaldo (Juventus).

Hata hivyo, Robert Lewandowski ambaye ni nahodha wa Poland ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA mwanaume mwaka wa 2020 baada ya mabao yake 55 ya msimu ambayo yemeisaidia Bayern Munich kutwaa mataji ya kimataifa na ya nyumbani.

Lewandowski alipata kura 52 dhidi ya 38 alizopata Lionel Messi wakati Cristiano Ronaldo akipata 35 huku Lucy Bronze wa Uingereza akishinda tuzo hiyo kwa upande wa wanawake.

Alishinda Ligi ya Mabingwa akiwa na Olympique Lyonnais kabla ya kuhamia Manchester City. Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alimpiku Mjerumani mwenzake Hansi Flick wa Bayern Munich na Marcelo Bielsa wa Leeds katika tuzo ya kocha bora. Manuel Neuer alishinda tuzo ya kipa bora. 

Licha ya hafla ya tuzo hiyo kufanyika Zurich, Uswisi kwa njia ya video, Rais wa FIFA, Gianni Infantino alikwenda hadi Munich kumkabidhi yeye mwenyewe Lewandowski tuzo yake hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news