Yanga yaichapa Mwadui FC 5-0

Unaweza kusema kwa sasa Wanajangwani, Yanga SC hawakamatiki katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuendeleza ushindi wake huku ikitoa dozi za mabao za kutosha,anaripoti Mwandishi Diramakini.

Ni baada ya leo Desemba 12, 2020 kuichapa 5-0 wenyeji, Mwadui FC katika Uwanja wa Kambarage uliopo mkoani Shinyanga.

Deus Kaseke dakika ya sita, mshambuliaji Mburkinabe Yacouba Sogne dakika ya 14 na 49 na winga Mkongo Tuisila Kisinda dakika ya 57 na beki Mghana, Lamine Moro dakika ya 70 ndio waliofunga hesabu hiyo.

Hivyo kwa ushindi huo, Yanga SC inayofundishwa na kocha Mrundi, Cedric Kaze imefikisha pointi 37 katika mechi ya 15 na sasa inaongoza Ligi Kuu kwa pointi 10 zaidi ya Azam FC inayofuatia, wakati mabingwa watetezi, Simba SC ni wa tatu wakiwa na pointi 26 za mechi 12.

LIVE TIZAMA HAPA

Mchezo huo umechezeshwa na Refa Ahmada Simba wa Kagera aliyesaidiwa na Rashid Zonga wa Iringa na Credo Mbiya wa Mbeya ambapo winga wa zamani wa AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kisinda alishindwa kumalizia mechi baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Ditram Nchimbi zikiwa zimebaki dakika 10 kabla ya kufunga pazia.

Hata hivyo, mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Polisi Tanzania imelazimishwa sare ya bila kufungana na Ruvu Shooting Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, wakati bao pekee la Seif Abdallah Karihe dakika ya 47 limeipa Dodoma Jiji FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Gwambina Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news