Mamilioni ya Watanzania na wageni kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki katika mkesha mkubwa maalum Kitaifa Desemba 31, 2020 anaripoti Mwandishi Diramakini.
Hayo yamebainishwa leo Desemba 29, 2020 na Askofu Dkt. Godfrey Emmanuel Malassy ambaye ni Mwenyekiti na Mbeba Maono Mkesha Mkubwa nchini.
"Sasa ni takribani miaka 23 tangu maono ya Mkesha Mkubwa Kitaifa Dua Maalum kuanza mnamo mwaka 1997 na kufanyika kila mwaka tarehe 31 Disemba, katika mikoa mbalimbali pamoja na Zanzibar.
"Hata hivyo tunayo sababu ya kufanya Dua Maalum kwa Taifa hasa kwa ajili ya kumshukuru Mungu kutupatia kiongozi mwenye uwezo,mcha Mungu,mkweli na asiyependa mapato ya aibu ili kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano kwa awamu ya pili.
"Tunamshukuru Mungu kwamba amesikia dua zetu Watanzania. Leo Watanzania na Ulimwengu mzima ni mashahidi wa matokeo chanya katika nyanja zote za maendeleo ya Taifa letu bila kusahau kudumishwa kwa amani na utulivu endelevu.
Amesema, katika tukio la kwanza, mwaka huu yeye (Askofu Dkt.Godfrey Emanuel Godfrey Mwenyekiti Mkesha Mkubwa Kitaifa -Dua Maalum) na viongozi wengine wa kiroho nchini wataongoza shukurani ya kipekee ya Kitaifa kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuponya na janga la Corona (COVID-19).
Janga ambalo limeikumba Dunia nzima, "sisi Watanzania tunayo sababu muhimu kumshukuru Mungu kutushindia na kutuepusha na janga hili hatari.
"Tukio la pili, mwaka huu lenye umuhimu kwa Taifa la Tanzania ni kumshururu Mungu kwa kutusaidia kutekeleza mchakato mzima wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kwa amani na utulivu endelevu, kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa,Dkt. John Pombe Jospeh Magufuli kwa jukumu kubwa alilokabidhiwa na kila Mtanzania kuongoza Taifa letu la Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano 2020 -2025.
"1 Timotheo 2:1–3..Tukio muhimu la tatu mwaka huu, ni kumshukru Mungu kwa kututendea kama Taifa katika nyanja ya kiuchumi, sasa Taifa letu limeingia rasmi katika orodha ya nchi zenye uchumi wa kati kabla ya wakati uliokosudiwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025.
"Haya ni baadhi ya maombi tuliokuwa tunaomba kupitia Mkesha huu kwa miaka mingi.Maono ya Mkesha Mkubwa Kitaifa -Dua Maalum kwa Taifa,yamelenga Taifa liwe na amani na utulivu endelevu toka kwa Mungu wa Amani aliye hai pamoja na ustawi wa Taifa na wananchi wote kwa ujumla bila kujali rangi, kabila, dini, wala itikadi.
"Watanzania tunatambua kwamba;1.Hakuna amani bila Mungu,yeye ndiye mtoa amani kwa watu wote wamchao kwa kusudi lake. Mungu analokusudi na Taifa hili na ndiyo maana ametoa amani hii,2Nyakati 7: 142. Hakuna mahali popote duniani Taifa lililomtegemea Mungu likashindwa.
"Amani ni msingi wa maisha ya mwanadamu. Bila amani maisha yanakuwa magumu. Mtu hana usalama na mtu mwingine, kazi na shughuli za kila siku zinakwama n.k. Taifa lisilo na amani haliwezi kusonga mbele kimaendeleo hata lifikie malengo yake. Karibuni wote,"Amesema Askofu.
Tags
Habari