Marekani kufungua Ubalozi mdogo Sahara ya Magharibi

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Mike, Pompeo amesema kuwa, Marekani imeanza utaratibu wa kufungua ubalozi mdogo katika Sahara ya Magharibi, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Waziri Pompeo ndiye alikuwa afisa wa kwanza wa juu wa Marekani kufanya ziara nchini Morocco baada ya Rais Donald Trump kuingia madarakani mwaka 2016.

Hatua hii imechukuliwa na serikali ya Marekani ikiwa ni wiki chache tu baada ya utawala wa Rais Donald Trump kutambua rasmi madai ya Morocco ya kumiliki koloni hilo la zamani la Uhispania. 

Koloni hilo linalogombaniwa na Chama cha Ukombozi cha Sahrawi ambapo kwa mujibu wa taarifa ya Waziri Pompeo ubalozi huo mdogo ambao hautakuwa na mtu huko utasimamiwa na ubalozi wa Marekani nchini Morocco. 

Hata hivyo, Morocco ilichukua udhibiti wa jimbo hilo la Sahara Magharibi mwaka 1975 baada ya mtawala wa kikoloni Uhispania kujiondoa na kusababisha mapigano ya chini kwa chini kwa ajili ya uhuru wa jimbo hilo ambayo yalimalizika mwaka 1991 wakati Umoja wa Mataifa ulipatanisha na kupeleka jeshi la kulinda amani katika jimbo hilo. 

Aidha, hatua hiyo pia ilikwenda sambamba na kufanyika kwa kura ya maoni kwa ajili ya kuamua hatma ya baadae ya eneo hilo ingawa kura hiyo ilitatizwa na mambo mengi.Wachambuzi wa masuala ya Kimataifa wanaeleza kuwa, Morocco inalichukulia eneo la Sahara Magharibi lenye utajiri mkubwa wa madini kama jimbo lake la Kusini na imependekeza kulipa eneo hilo nguvu kubwa ya kujitawala nchini humo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news