Mhandisi Maganga ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu REA

Bodi ya Nishati Vijijini (REB) katika kikao kilichofanyika Desemba 20, 2020 imemteua Mhandisi Amos William Maganga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuanzia tarehe 16 Desemba 2020 kwa mujibu wa kifungu cha 25(1) cha Sheria Namba 8 ya Nishati Vijijini ya mwaka 2005, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mhandisi Amos William Maganga 

Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Maganga alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA. Mhandisi Maganga ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika sekta ya nishati. Aidha, ameshika nyadhifa mbalimbali toka alipokua ameajiriwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). 

Bodi inaomba ushirikiano kutoka kwa wadau wote ili kumuwezesha Mhandisi Maganga kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Wakala.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news