Jumla ya wanafunzi 37,834 sawa na asilimia 82.5 wametangazwa kufaulu mtihani wa darasa la Saba katika mkoa wa Geita uliofanyika mwaka huu huku Wilaya ya Bukombe ikishika nafasi ya kwanza kimkoa na Halmashauri ya Wilaya Geita ikishika nafasi ya mwisho kimkoa,anaripoti Robert Kalokola (Diramakini) Geita.
Fadhili Juma (katikati) ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Constantine Morandi (kushoto) na Thomas Dime, Katibu Tawala Wilaya ya Geita (kulia) wakishiriki katika kikao cha kutangaza matokeo ya darasa la saba mkoa wa Geita. (Picha na Robert Kalokola/ Diramakini).
Mkoa wa Geita ulisajili watahiniwa (wanafunzi) wa darasa la Saba kwa ajili ya kufanya mtihani wa darasa la saba 47,444, lakini waliofanya mtihani ni 46,031,wavulana wakiwa 22,666 na wasichana 23,365 ambapo wanafunzi 1,413 walishindwa kufanya mtihani huo kutokana na utoro,ugonjwa,vifo na sababu nyingine.
Akitangaza matokeo hayo na shule walizopangiwa wanafunzi hao katika kikao maalum kilicho shirikisha kamati ya mitihani ya mkoa,wakuu wa wilaya zote, wakurugenzi wa halmashauri,wenyeviti wa halmashauri,maafisa elimu wilaya na wadau wa elimu, Afisa Elimu wa Mkoa wa Geita, Anold Msuya amesema ufaulu katika ngazi ya mkoa umepanda kwa asilimia tatu kutoka asilimia 79.12 mwaka 2019 hadi asilimia 82.50 mwaka huu.
Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Katibu tawala wa kikao hicho amewaomba viongozi kutoka wilaya zote ndani ya mkoa kusimamia vizuri watumishi wa idara za elimu hasa walimu ili wafundishe na matokeo yaendelee kuwa mazuri kimkoa.
Denis Bandisa Katibu Tawala Mkoa wa Geita (katikati) na Anold Msuya (kushoto) Afisa Elimu Mkoa wa Geita wakishiriki kikao cha kutangaza matokeo ya darasa la saba Mkoa wa Geita, (Picha Robert Kalokola).
Ameshauri kutumia wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuboresha elimu katika halmashauri zao hasa kwa kuwatia hamasa za kufundisha kwa bidii.
Afisa Elimu Msuya ametaja halmashauri iliyofanya vizuri katika mkoa kuwa ni Bukombe (93.3%), ikifuatiwa na Geita mji (90.6), Halmashauri ya wilaya ya chato (86.5%), Nyang'hwale (85.5%),Mbogwe (83.7%) na Mwisho ni Halmashauri ya Wilaya ya Geita (82.5%).
Msuya amesema kuwa, mwenendo wa ufaulu kimkoa umekuwa ukipanda kila mwaka ambapo mwaka 2012 mkoa ulikuwa na wastani wa 31.00% ,lakini umekuwa ukipanda hadi mwaka huu 82.50%.
Ametaja shule 10 bora katika mkoa ambazo zote ni shule zinazo milikiwa na watu binafsi ndani ya mkoa kutoka wilaya tofauti tofauti.
Shule hizo ya kwanza ni Citizen (Bukombe), ya pili ni Samandito(Geita mji),ya tatu Hwima Mine(Bukombe), ya nne St.Padre Pio (Bukombe),ya tano ni Royal Family (Geita mji) ,ya sita ni Waja Springs (Geita mji),Saba ni Golden ridge (Geita mji), Nane ni Paradise English Medium (Chato),tisa ni Golden valley (Geita mji) na mwisho ni Noble Bridge (Geita mji).
Mariam Chaurembo (aliyesimama) Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyang'hwale akichangia hoja katika kikao cha kutangaza matokeo ya darasa la saba na kujadiliana namna ya kuboresha elimu na kupata matokeo mazuri kimkoa. (Picha na Robert Kalokola/ Diramakini).
Pia amezitaja shule 10 zilizo shika nafasi za mwisho kimkoa kuwa ni shule ya Msingi Mponda(Mbogwe),Isabilo(Geita),Luhula(Mbogwe),Shahende(Geita),Ng'wabagagalu(Geita),Chabulongo(Chato),Nyakasenya(Geita),Buzanaki(Geita),Nyakamwaga(Geita) na Mwisho ni shule ya Msingi Kaduda(Geita).
Aidha, Afisa elimu Anold Msuya aliwataja wanafunzi 10 bora kimkoa waliofanya vizuri kuwa ni Emmanuel Ramadhan Juma kutoka shule ya Samandito mjini Geita amepata alama 246 kati 250 na kupangiwa Tabora boys.
Mwanafunzi mvulana wa pili ni Edson Tengo Buzabulambu shule ya Samandito (246) amepangiwa Tabora boys, Samson Tengo Buzabulambu Samandito (245) amepangiwa Mzumbe.
Wengine ni Christopher Cosmas Shija, shule ya Citizen (245) amepangiwa Tabora boys,Kayange Sitta Kabosolo shule ya Citizen (244) amepangiwa Tabora boys,Josephat Jovin Leonard kutoka shule ya Citizen (244) amepangiwa Mzumbe na Rodrick David Isack shule ya Samandito (244) amepangiwa Tabora boys.
Wengine ni Shem Gabriel Lazaro shule ya Citizen (243) amepangiwa Tabora boys, Gilbert Muganyizi Mutalemwa wa shule ya Paradise (239) amepangiwa Mzumbe na Mwisho ni Juma Magembe Juma wa shule vya Kinsabe (239) amepangiwa Tabora boys.
Wasichana 10 bora kimkoa waliotangazwa leo na Afisa Elimu Anold Msuya ni pamoja na Janeth malau majula shule ya Samandito (246) Tabora girls', Sada Ramadhan Elias , Samandito(246) amepangiwa Msalato.
Wengine ni Happyness Rhuby Rokomo Samandito (245) amepangiwa Tabora girls', Josephine Wayala Msuka kutoka shule ya Msingi citizen (243) amepangiwa Msalato,Perusi Bwire Sylvester shule ya Citizen (243) amepangiwa Tabora girls', Angel Festo Bazila shule ya Uyovu (241) amepangiwa Tabora girls.
Wasichana wengine ni Levina Samwel Aron kutoka shule ya Paradise (238) amepangiwa Msalato,Laurencia Joseph Bushesha shule ya Paradise (234) amepangiwa Tabora girls',Helena Basi Julius shule ya Msingi Paradise (234) amepangiwa Msalato na Mwisho ni Muhindi Nyarenda Nyamhocha shule ya Msingi Nyang'hwale (225) amepangiwa Msalato.
Licha cha ufaulu kuongezeka shule ya Msingi Ushirombo Wilaya ya Bukombe wanafunzi 165 walifutiwa matokeo yao ya darasa la Saba mwaka huu wavulana wakiwa 70 na wasichana 95 na wanafunzi wawili kutoka wilaya ya Geita na chato kwa makosa ya udanganyifu wa mitihani.
Tags
Habari