Mr.Kuku ahukumiwa jela, ukwasi wa Bilioni 5.4 kuhamishiwa akaunti ya DPP

Mahakama ya Hakimu Mkazi imemhukumu mfanyabiashara Tariq Machibya (Mr. Kuku) kulipa faini ya sh. milioni 5 au kwenda jela miaka 5 baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mawili, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kwa mujibu wa Mahakama makosa hayo ni kujihusisha na biashara ya upatu kwa kukusanya fedha kutoka kwa umma na kukubali kupokea miamala ya fedha bila ya leseni.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Isaya, baada ya upande wa Jamhuri kuingia makubaliano ya kulipa kiasi hicho.

Aidha, katika hukumu hiyo, Mr. Kuku amehukumiwa kulipa faini ya sh. milioni 2 au kifungo cha miaka 5 na katika kosa la pili ametakiwa kulipa faini ya sh. milioni 3 au kifungo cha miaka 5.

Kwa mujibu wa Mahakama ikiwa atashindwa kulipa faini, vifungo vyote vitaenda sambamba. 

Pia mahakama hiyo, imemuamuru fedha sh. bilioni 5.4 ambazo zipo Benki ya CRDB kwenye akaunti ya mshitakiwa huyo kwenda kwenye akaunti ya Mkurugenzi ya Mashitaka nchini( DPP) iliyoko Benki Kuu ya Tanzania(BoT).

Hakimu Isaya amesema mshitakiwa anamtia hatiani kama alivyoshitakiwa ambapo mshitakiwa ameshindwa kulipa fedha hizo na amepelekwa rumande.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news