Msanii maarufu wa Bongo Movie hapa nchini Mohammed Fungafunga aliyekuwa maarufu katika tasnia hiyo kwa jina la maarufu la Jengua (pichani) amefariki dunia leo Desemba 15, 2020, Mkuranga mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa taarifa, Marehemu Jengua alikua akisumbuliwa na maradhi ya kupooza.
Enzi za uhai wake, Mzee Jengua aliigiza maigizo mbalimbali ya kuvutia kama Kidedea, Handsome wa Kijiji, na Kashinde.
Katibu wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Dar es Salaam, Doricy Kente amesema Mke wa Msanii huyo amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, chanzo cha kifo bado hakijatajwa. Endelea kufuatilia hapa kwa taarifa zaidi.