Orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2021

Jumla ya wanafunzi 759,706 sawa na asilimia 91.1 ya wanafunzi waliofaulu wakiwemo wavulana 368,174 na wasichana 391,532 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2021,anaripoti Mwandishi Diramakini.

Kauli hiyo imebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo wakati akitoa taarfa ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2021 jijini Dodoma.

Akizungumza Mhe. Jafo amesema kuwa kati ya wanafunzi 4,169 wamechaguliwa kujiunga na shule za bweni ambapo wanafunzi 970 watajiunga na shule za wanafunzi wenye ufaulu mzuri Zaidi.

Pia Mhe. Jafo amesema kuwa wanafunzi 1,238 watajiunga na shule za ufundi, wanafunzi 1,961 watajiunga na shule za bweni za kawaida.

Wanafunzi 755,537 wakiwemo wavulana 362,247 na wasichana 385,665 wamechaguliwa kujiunga na shule za Sekondari za kutwa katika maeneo mbali mbali nchini.

Hii hapa ni Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza Tanzania Bara kwa mwaka 2021, bonyeza kila mkoa uweze kujisomea hapa chini;

OFISI YA RAIS - TAMISEMI

UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA, 2021

CHAGUA MKOA ULIKOSOMA

ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA
GEITA IRINGA KAGERA
KATAVI KIGOMA KILIMANJARO
LINDI MANYARA MARA
MBEYA MOROGORO MTWARA
MWANZA NJOMBE PWANI
RUKWA RUVUMA SHINYANGA
SIMIYU SINGIDA SONGWE
TABORA TANGA

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news