Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Shukrani E. Manya kuwa Naibu Waziri wa Madini.Profesa Manya alikua Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Tanzania. Pia, ameteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ataapishwa leo mchana Chamwino, jijini Dodoma kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu.
Tags
Habari