Rais Magufuli akagua ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi aeleza alivyonusurika kuzama maji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Joseph Magufuli leo Desemba 28,2020 amekagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigongo–Busisi ambalo litakuwa na urefu wa kilomita 3.2 na litakua ndio daraja refu kuliko yote Afrika Mashariki na Kati, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Daraja hilo ambalo linajengwa na Mkandarasi wa China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) kwa gharama ya karibu sh. Bilioni 700, linatarajiwa kukamilika Februari 2024 na tayari ujenzi umefikia asilimia 11.18.

Rais Magufuli amefurahishwa na hatua iliyofikiwa, lakini amemtaka Mkandarasi huyo kuongeza kasi ya ujenzi kwa kufanya kazi usiku na mchana ili likamilike haraka na kuanza kutumika.

Dkt.Magufuli amesema, daraja hilo lina umuhimu mkubwa kwa Watanzania na Uganda, Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Pia amesema kuna kisa cha kuhuzunisha ambacho ndio kilimfanya aweke dhamira ya kuhakikisha hilo daraja linajengwa. 

Rais amesema, yeye ni mmoja wa walionusurika kufa maji baada ya mtumbwi ambao alikataa kuupanda kuzama na kusababisha vifo vya watu 11 waliokubali kupanda mtumbwi huo ili kuvuka kutoka Busisi kwenda Kigongo.



Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news