Rais mstaafu Dkt. Kikwete amshauri Manara, mkewe kuvumiliana

Desemba 10, 2020 Afisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara amefunga ndoa na mkewe Naheeda katika Msikiti wa Masjid Maamur jijini Dar es Salaam huku wakipewa wosia utakaowawezesha kulistawisha penzi lao daima, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Ndoa yake imehudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Rais mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum na watu wengine wengi maarufu hapa nchini.

Dkt.Kikwete amesema kuwa, Haji alimfuata nyumbani na kumshirikisha jambo hilo kwa ajili ya ndoa na akamuahidi kufika."Hakuna ufundi kwenye ndoa, kikubwa ni kustahimiliana na kuvumiliana.
"Mnapaswa kuwa makini na kusikilizana katika ndoa, pia nakushauri kwamba uwe na uvumilivu na kuona namna gani mnaweza kuleta watoto kwa kuulizana na kujua mambo yatakuaje.

"Baraka za Mungu kwa watoto ni zake kwa kadri atakavyoamua, yale makundi yaache kwa kuwa kila mmoja anajua anachokipenda. Nilikuwa ninazungumza na mzee hapo nyuma akaniambia kwamba anahitaji wajukuu hivyo ni jambo la kheri na linahitaji subira kikubwa ninawapongeza katika hilo na ninaamini kwamba itakuwa kheri,"amesema Dkt.Jakaya Kikwete.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news