Rais Museveni ataja kitakachomfanya kusalia madarakani tena na tena

Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ambaye anawania muhula wa sita madarakani amesema bado hajaona mtu mwenye uwezo wa kuongoza Uganda kwa sasa, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mzee Museveni amesema kwa msingi huo ataendelea kuwa madarakani kwa sababu wapiga kura nchini humo bado wanamhitaji kuendelea kuongoza taifa hilo ili kuwaletea maendeleo na kudumisha amani.
Museveni ameyasema hayo wakati akiwahutubia viongozi wa chama chake cha National Resistance Movement (NRM) katika wilaya ya Lukungiri.

Wilaya ambayo ni ngome ya kisiasa ya aliyekuwa mpinzani wake mkuu mara nne na ambaye kwa sasa yupo kimya,Dkt. Kiiza Besigye.

Rais Museveni amesema kwamba wapinzani wake ni watu wazembe wanaotaka kusukumwa kama mkokoteni, hivyo haoni ambaye anaweza kuiongoza Uganda.

Kati ya wapinzani wake 10 katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao 2021, ni waliokuwa makamanda muhimu wakati walipokuwa msituni katika vita vilivyomwezesha kuingia madarakani mwaka 1985.

Wagombea hao ni Luteni Jenerali Henry Tumukunde na aliyekuwa Kamanda Mkuu wa Jeshi Meja Jenerali Mugisha Muntu.

Dkt. Kiiza Besigye si mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, lakini anamfanyia kampeni mgombea wa chama chake cha Forum for Democratic Change Patrick Amuriat.

Aidha, Dkt.Besigye, Tumukunde na Muntu, wanaendelea kufanya kampeni katika sehemu kadhaa za Uganda wakimtaka Rais Museveni kuondoka madarakani wakisema kwamba ameshindwa kutekeleza sababu kuu zilizowafanya kuingia msituni na kuanzisha vita vilivyomwezesha Museveni kuingia madarakani.

Lakini Museveni amesema kwamba wanaomkosoa walishindwa na kazi licha ya kujaribu kila mara kuwaweka katika sehemu tofauti serikalini na sasa wanampigia kelele.

Amesema, wanajua lengo lake katika siasa lakini wanataka kunishawishi niache msimamo wangu. Wanapiga kelele kwamba nastahili kuondoka madarakani utadhani sina pa kwenda,” amesema Museveni akitumia mojawapo ya lugha zinazozungumzwa magharibi mwa Uganda.

Akiwataja watatu hao ambao walikuwa marafiki wake wa muda mrefu na mmoja alikuwa daktari wake binafsi akimaanisha Dkt. Kiiza Besigye kuwa no watu wasiokuwa na maana yoyote na ambao sasa wanataka aondoke madarakani.

Amesema kwamba, huwa anakasirika sana anaposikia watu wakimuambia kwamba aiondoke madarakani, lakini huwa anajaribu sana kujizuia na kuwa mtulivu.

“Kama ulishindwa kufanya nilichokuambia, usilete vurugu kwa kuniambia kwamba niondoke madarakani. Wapiga kura ndio wanaoamua.

"Hata nikiondoka nani hao wasiokuwa na maana yoyote ambao wanataka kusukumwa kama mkokoteni wanaotaka kuongoza nchi hii. Muniache niendelee kuongoza kwa sababu raia wa Uganda wananihitaji niwepo. Nitaondoka tu iwapo kuna mtu wa maana nitakayeona naweza kumuachia Uganda. Nataka niwe na uhakika mahali naiacha Uganda,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news