Real Madrid ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Hispania wamefanikiwa kuondoka na alama tatu muhimu katika mchezo wa 'derby' dhidi ya Atletico Madrid, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Picha na GIUSEPPE CACACE/AFP via Getty Images.
Mtanange huo umechezwa katika uwanja wa la Alfredo Di Stefano Desemba 12, 2020 ambapo matokeo yalikuwa ni mbili kwa sufuri.
Bao la Casemiro ndani ya 15 akimalizia kona ya kiungo mshambuliaji Toni Kroos liliwapa uongozi kabla ya makosa binafsi ya mlinda mlango wa Atletico, Jan Oblak kupeleka Real kupata goli la pili ambalo liliumaliza mchezo kabisa ndani ya dakika tisini.
Jan Oblak alishindwa kuukoa shuti la Dani Carvajal ambalo liligonga mwamba na kumgonga yeye mwenyewe na kuingia moja kwa moja katika nyavu.

Real Madrid ambao wapo nafasi ya tatu katika msimamo wa La Liga kupitia matokeo hayo yanaifanya kuwa nyuma kwa alama tatu pekee juu ya vinara Atletico ambao wamekuwa wakiongoza msimamo wa La Liga.
Tags
Michezo