Ridhiwani Kikwete:Chalinze hakuna kulala, ni mwendo wa kazi

Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete amesema muda wa kazi ni sasa, hakuna kulala wala likizo ili kuwatumikia Watanzania wanyonge, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Ridhiwani ambaye amekuwa katika shughuli mbalimbali za kijimbo, ambapo  Desemba 27, 2020 licha ya kuwa ni siku ya mapumziko, ameweza kufanya ziara ikiwemo kukagua shule za sekondari zaidi ya sita pamoja na ukaguzi wa soko la kisasa linalojengwa Bwilingu-Chalinze Mjini.

Awali akikagua soko hilo na kujionea maendeleo yake pia aliweza kuonana na baadhi ya wafanyabiashara wakiwemo jumuiya ya wachinjaji kuku na nyama.

"Mkandarasi ametuhakikishia ujenzi unaendelea vizuri na kwa kasi. Pia nimepata kukagua vizimba vyake katika soko hili ambalo litakuwa kitega uchumi ndani ya Halmashauri yetu.

"Soko hili ni moja ya utekelezaji wa ilani ambao unakwenda sio tu kuupa sura mji wa Chalinze lakini unakwenda kubadilisha na maisha ya watumiaji wa soko na njia tunazofanya biashara,"amesema Ridhiwani Kikwete.

Mbali na ukaguzi wa soko hilo, pia Ridhiwani Kikwete amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani na Maagizo ya viongozi kuhusu mustakabali wa Tanzania ya agenda ya Elimu huku akiambatana na Watendaji wa Idara ya Elimu Sekondari na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze, Ramadhani Possi.

"Tumetembelea shule 6 ikiwemo shule ya sekondari Chalinze, Chahua,Msata, Kiwangwa, Changalikwa, Rupungwi na Mandela wasichana.

"Tumeshuhudia maendeleo makubwa yaliyokwisha fanyika ikiwemo ujenzi wa madarasa, mabweni na ofisi za walimu,"amesema Ridhiwani Kikwete.

Mbali na hayo Mbunge ameshuhudia ujenzi wa madarasa 17 unaoendelea katika maeneo mbalimbali yanayotaraji kukamilika kabla ya tarehe 17 ili yawe tayari kutumiwa katika mwaka mpya wa elimu. Ziara ya Mbunge inaendelea katika Kata mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news