Ujumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki umetembelea mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa lengo la kijionea maendeleo ya ujenzi wa maradi huo unaotekelezwa hapa nchini, anaripoti Mwandishi Maalum Diramakini.
Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala, Mhandisi Steven Mlote akifualia mada iliyokuwa ikiwalishwa na mtalaamu wa ujenzi kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa mradi wa treni ya kisasa (SGR) mara baada ya kuwasili katika eneo la Makutupola jijini Dodoma.
Ujumbe huo ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala, Mhandisi Steven Mlote ulianza safari ya kutembelea mradi huo kuanzi Makutopola hadi Dar es Salaam.
Ujumbe ulipata fursa ya kujionea hatua ya maendeleo iliyofikiwa sambamba na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na katika utelezaji wa mradi, ikiwemo viwanda vya kuzalishia baadhi vifaa vinavyotumika katika ujenzi wa mradi.
Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhandisi Steven Mlote akiwa na Mhandisi Ignas Lymo kutoka Shirika la Reli Tanzania wakitokea kwenye moja ya handaki (tunnel) la kupita treni.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhandisi Mlote amesema amefurahishwa na kazi kubwa inayofanywa na Serikali katika kutekeleza mradi huo ambao unamanufaa makubwa kwa Taifa na kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
“Tuemeona kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuteleza mradi huu mkubwa, tunampongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa kubuni mradi huu,”amesema Mhandisi Mlote.
Aidha, ameongezea kuwa, amefurahishwa na ushiriki wa idadi kubwa ya vijana wa Kitanzania katika sekta mbalimbali za ujenzi wa mradi huo ulioajiri takribani watu 13,796.
Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhandisi Steven Mlote (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watalumu wa ujenzi na Watumishi wa Shirika la Reli Tanzania nje ya handaki (tunnel) la kupia treni.
Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhandisi Steven Mlote akifualia mada iliyokuwa ikiwalishwa na mtalaamu wa ujenzi kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa mradi wa treni ya kisasa (SGR) mara baada ya kuwasili katika eneo la kambi ya Soga mkoani Pwani.
Amewasihi vijana wa Kitanzania waliopata fursa ya ujenzi wa reli kuendelea kujifunza kwa moyo na kwa kujituma ili kupata maarifa na ujunzi wa kuendelea kutunza, kuendesha na kuendeleza mradi huo hata baada ya wataalmu kutoka kampuni inayohusika na ujenzi kuondoka nchi.Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhandisi Steven Mlote akitembea pembezoni mwa reli ambayo ipo katika hatua za mwisho za ujenzi.
Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhandisi Steven Mlote akijadili jambo na watalamu wa ujenzi wa reli ya kisasa alipo tembelea ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhandisi Steven Mlote akisikiliza malezo kutoka kwa Mhandisi Ignas Lyimo kutoka Shirika la Reli Tanzania alipotembelea Stesheni ya Treni ya Morogoro mjini.
Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhandisi Steven Mlote akiendelea kusikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi Ignas Lyimo kutoka Shirika la Reli Tanzania alipotembelea Stesheni ya Treni ya Morogoro mjini.Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhandisi Steven Mlote akisikiliza maelezo kutoka kwa mataalamu alipotembelea Stesheni ya Treni ya iliyopo eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
Kwa upande mwingine, Mhandis Mlote ametoa wito kwa Watanzania hasa ambao wanazunguka eneo la mrafi, wikuanza kujiandaa kikamilifu katika kunufaika na fursa zitakazotokana na mradi wa reli ya kisasa kwa kuanza kuongeza uzalisha wa mazao shambani na bidhaa za viwandani kwa kuwa mradi huo utarahisisha usafirishaji wa bidhaa na watu kwenda nchi jirani za Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Nchi za Afrika ya Kati.
Ujumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pia unatarajia kutembelea mradi wa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere, lililopo Wilayani Rufiji kwa lengo la kujionea hatua iliyofikiwa katika ujenzi.