Serikali yaazimia kuendeleza Sekta ya Sanaa nchini

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amewataka wakuu wa taasisi zinazosimamia Sekta ya Sanaa nchi kuandaa mikakati itakayosaidia kukuza na kuendeleza sekta hiyo, anaripoti Anitha Jonas (WHUSM), Dar es Salaam.

Dkt. Abbasi ametoa kauli hiyo Novemba 30, 2020 jijini Dar es Salaam katika kikao na viongozi chenye lengo la kutafuta suluhu ya namna bora ya kuendeleza Sekta ya Sanaa nchini.  

Katika kikao hicho Katibu Mkuu huyo alisisitiza kuwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika hotuba yake mara baada ya kuapishwa na katika ufunguzi wa Bunge pamoja na katika Ilani ameeleza lengo la kuendeleza Sekta ya Sanaa.  

Akizungumza katika kikao hicho kilichokuwa na wakuu kutoka BASATA, COSOTA, Bodi ya Filamu na TaSuBa amesisitiza kuwa, lazima Sekta ya Sanaa ijipange kuwa na miundombinu mbinu yake ya kisasa itakayoendeleza kazi hiyo ikiwemo ujenzi wa “sport arena”.  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akitoa maagizo kwa Watendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania kuratibu ushiriki wa Wasanii wa Filamu na BASATA kuratibu ushiriki wa Wasanii wa Muziki katika kazi za serikali kwa lengo la kuepuka mawakala wanaoleta migogoro miongoni mwao Novemba 30,2020 jijini Dar es Salaam katika kikao na wakuu wa taasisi zinazosimamia sekta ya sanaa nchini .

“Sasa ni wakati wa kuangalia namna ya kutatua changamoto za kisekta na siyo changamoto binafsi tuangalie mambo gani yaboreshwe kama ni Sera, Sheria au Kanuni,”amesema Dkt.Abbasi.  

Pamoja na hayo, Dkt. Abbasi ametoa maagizo mbalimbali kwa Wakuu hao ikiwemo kuandaa mpango wa kutoka mafunzo mbalimbali, na kwa TaSUBa kujipanga kuwa na kozi za muda mfupi utoaji zitakazosaidia wasanii.

Vilevile Katibu Mkuu huyo alitoa maagizo kwa Bodi ya Filamu kusimamia na kuratibu shughuli zote za Serikali zitakazohitaji na Wasanii Wafilamu na kwa upande wa Muziki BASATA nao ndiyo kuwa waratibu hii ni kwa lengo la kuondoa mawakala miongoni mwao ambao huchangia kuleta changamoto mbalimbali.  Mtendaji Mkuu Taasisi ya Hakimiliki na Hakishiriki (COSOTA), Doreen Sinare akimshukuru Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi (hayupo pichani ) kwa kuwasaidia kupata mdau wa usambazaji kutoka India atakayeshirikiana wasambazaji wa filamu nchini wanaofanya tafsiri ya filamu za Kihindi.Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa Tanzania, Godfrey Mngereza akimshukuru Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi kwa maelekezo aliyoyatoa kwa baraza kuratibu ushiriki wa wasanii wa muziki katika shughuli za serikali , Novemba 30, 2020 jijini Dar es Salaam katika kikao na wakuu wa taasisi zinazosimamia sekta ya sanaa nchini.

Aidha, Dkt. Abbasi pia ameitakaTaasisi ya COSOTA kutafuta mfumo bora wa kieletroniki utakaosaidia ukusanyaji wa mapato ya kazi za wasanii pamoja na namna bora ya kutumia mifumo ya kidijitali katika kulinda haki za wasanii ili waweze kufaidika na kazi zao.  

Kwa upande wa Mtendaji Mkuu COSOTA, Doreen Sinare amemshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kupata wadau kutoka India, ambao watashirikiana na wasambazi wa kazi za filamu Tanzania ambao wanafanya tafsiri ya filamu za Kihindi ili kupata ridhaa ya wamiliki wa filamu za India zifanyiwe tafsiri

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news