Serikali yaidhinisha Mkutano Mkuu wa Diaspora ukaofanyika Dodoma

Serikali ya Jamhuri ya Muungano w a Tanzania imeidhinisha Mkutano Mkuu wa Baraza la Diaspora Watanzania Duniani (TDC Global) ambao unatarajiwa kufanyika Juni 23 hadi 26, 2021 jijini Dodoma, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mkutano huo ambao utafanyika makao makuu ya nchi unatarajiwa kuwakutanisha Watanzania mbalimbali kutoka kila kona ya Dunia. 

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Mahusiano ya Umma kutoka TDC Global, Bi. Agness P. Lerdorf huku akichukua nafasi hiyo kuipongeza Serikali kwa kuendelea kuwaunga mkono ili kufikia malengo ya kuwaunganisha Watanzania, hatua mbayo inatajwa itawezesha ushiriki wao kwa namna moja au nyingine kuwezesha kulisaidia Taifa kuyafikia matokeo chanya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news