Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Simai Mohammed Said amesema wizara yake itaendelea kushirikiana na wadau wote wa elimu ili kuhakikisha Taifa linazalisha wataalamu wa fani mbalimbali nchini, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Akizungumza wakati wa mahafali ya kwanza ya wanafunzi wa maandalizi wa Skuli ya Leera iliyopo Mbweni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja amesema, skuli binafsi nazo ni miongoni mwa wadau wakubwa wa elimu katika ngazi mbalimbali.
Mhe. Simai amewataka wamiliki wa skuli binafsi nao kubadilishana mawazo na Skuli za Serikali ikiwemo kushindana katika michezo mbalimbali na midahalo kwa masomo tofauti ili kuendelea kuinua sekta hiyo.
Aidha, Mhe. Waziri amewasisitiza wazazi na walezi kuhakikisha wanawaelekeza watoto wao katika elimu kwani elimu ni utajiri usioisha maishani mwao.
Hata hivyo amewasisitiza wamiliki wote wa skuli binafsi kuhakikisha wanawawekea usalama Wanafunzi hasa katika suala la usafiri kwa kuacha kuwajaza wanafunzi katika basi bila kiwango maalumu.
Pia ametoa agizo kwa wazazi kutoruhusu watoto wao kutumia vyombo vya moto wakiwa katika umri wa chini ya miaka 18,na kutoa angalizo ifikapo Januari wizara yake itaanzisha utaratibu maalum wa kuzuia watoto kutumia vyombo vya moto kwa umri mdogo.
Aidha, Mhe. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar amesema wizara yake itandaa uratibu maalum wa uvaaji wa majoho wakati wa mahafali katika ngazi mbalimbali ili kulipa heshima yake vazi hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Skuli ya Leera, Bwana Suleiman Rashid Mohd amesema mwalimu ni mtu mwenye thamani ya pekee ulimwenguni kutokana na kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja ikiwemo kusomesha na kulea ili taifa lizalishe wataalamu wenye nidhamu.
Jumla ya wanafunzi 17 wamehitimu masomo yao kwa ngazi ya maandalizi katika Skuli ya Leera iliyopo mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Tags
Zanzibar