Waziri Wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Simai Mohammed Said amewataka wazazi na walezi kuzidisha ushirikiano baina yao na walimu kwa lengo kuwajenga wanafunzi kuweza kufaulu vizuri katika mitihani yao ya Taifa, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Akizungumza katika Mahafali ya Pili ya Kidato cha Nne ya Skuli ya Turkish Maarif huko Kidimni Mkoa Kusini Unguja ameeleza kuwa, ili mwanafunzi aweze kufaulu vizuri katika masomo yake ni lazima uwepo ushirikiano mzuri baina ya wazazi, walimu na wanafunzi.
Aidha, amewataka wazazi wa kiume kujitahidi katika kushirikiana katika malezi ya watoto wao na kuwataka kushiriki vyema katika vikao vya wazazi wakati wanapohitajika Skuli ili kuweza kujua mwenendo wa watoto wao pamoja na maendeleo ya masomo yao.
Aidha, Mhe. Simai ametoa wito kwa wale wote ambao wanaofanya ukarabati au kujenga Skuli mpya kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi ambayo yatakuwa ni miongoni mwa njia za kujifunzia mambo ya sayansi.
Hata hivyo, ameeleza kuwa Wizara ya Elimu itaendelea kushirikiana na uongozi wa Skuli hiyo katika kufanikisha lengo walilojipangia pamoja na kuwapongeza kwa uamuzi mzuri waliouchukuwa wa kuwapunguzia ada Wanafunzi wote ambao ni mayatima na wenye hali ngumu ya kimaisha
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maarif, Ogumza Yilmaz amewapongeza wanafunzi wa Maarif kwa kuwa wastahamilivu katika kipindi chote cha korona kwa kusoma kupitia mitandao na kuwatakia mafanikio mema katika masomo yao yao ya badaae.
Pia ameeleza kuwa, wanatoa elimu kwa watoto wadogo ili waweze kujifunza mapema na kuweza kupata ujuzi mzuri wakati wakiwa bado watoto wadogo.
Jumuiya ya Turkish Maarif mefanikiwa kuanzisha Skuli nne Tanzania zikiwemo mbili za Zanzibar, moja Mkoa na moja ipo jijini Dar es Salaam.
Wakati huo huo Mhe. Simai alitembelea katika Skuli ya International iliyopo Mbweni Mjini Unguja na kufanikiwa kuona bidhaa mbalimbali za asili zilizotengenezwa na wanafunzi pamoja na makampuni na kujionea michezo na vipaji mbali mbali vya wanafunzi hao.
Mhe. Simai alifanya ziara hiyo skuli hapo ikiwa ni siku yao maalum ya maonesho na kuwataka wanachi kufika katika Skuli hiyo ili waweze kufadika na kuweza kujifunza mambo mbalimbali.

Tags
Zanzibar