Kamati Tendaji ya Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari (MAELEZO) wamejipanga kufanikisha Kikao Kazi cha Maafisa Habari kinachotarajiwa kufanyika Machi 2021 jijini Mbeya, anaripoti Mwandishi Maalum Diramakini (MAELEZO).
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Rodney Thadeus akieleza jambo kwa wajumbe wa Kamati Tendaji ya TAGCO leo Desemba 18, 2020 mjini Morogoro kuhusu hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini mwaka 2021.
Kikao cha kuweka mikakati ya kufanikisha kikao kazi hicho kimefanyika mjini Morogoro Desemba 18 na 19, 2020 na kuongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Bi. Sara Kibonde ambapo kilitanguliwa na ziara ya wajumbe hao katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma ambapo walitembelea halmashauri hiyo ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake kuwatembelea maafisa habari ili kujionea utendaji wao.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari Serikalini (TAGCO), Bi. Sara Kibonde akiongoza kikao cha Kamati Tendaji ya chama hicho na Idara ya Habari (MELEZO) mjini Morogoro Desemba 18 na 19 , 2020 kikilenga kujadili pamoja na mambo mengine maandalizi ya Kikao Kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kinachotarajiwa kufanyika Machi 2021 jijini Mbeya.
Kikao hicho kimefanyika ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa TAGCO na Idara ya Habari- MAELEZO kushirikiana katika maandalizi na hatimaye kufanikisha kikao kazi hicho kinachofanyika kila mwaka na kushirikisha maafisa habari kutoka katika Wizara, Mikoa,Halmashauri, Taasisi na Idara za Serikali zinazojitegemea.
Mjumbe wa Kamati Tendaji ya TAGCO, Dkt. Cosmas Mwaisobwa (wa kwanza kushoto) akieleza jambo kwa wajumbe wa Kamati hiyo Desemba 18, 2020 mjini Morogoro wakati wa kikao cha maandalizi ya kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kinachotarajiwa kufanyika Machi 2021 jijini Mbeya.
Kwa mwaka 2021 TAGCO kwa kushirikiana na Idara ya Habari MAELEZO inaratibu kikao hicho kitakachoshirikisha zaidi ya mafisa habari 400 .
Aidha, mada mbalimbali zitawasilishwa zikilenga kuwajengea uwezo maafisa habari ili waweze kutekeleza dhana ya mawasiliano ya kimkakati katika kuandika na kuripoti habari za miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao katika kipindi cha pili cha Serikali ya Awamu ya Tano.
Wajumbe wa Kamati Tendaji ya TAGCO wakifuatilia kikao cha maandalizi ya Kikao Kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kwa kinachotarajiwa kufanyika Machi 2021 jijini Mbeya.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Bi. Zamaradi Kawawa akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja kati ya TAGCO na Idara ya Habari (MAELEZO) kilichofanyika mjini Morogoro Desemba 18 na 19,2020 kwa lengo la kujadili na kuweka mikakati ya kufanikisha kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kinachotarajiwa kufanyika Machi 2021 jijini Mbeya.
Katibu Mtendaji wa TAGCO, Bw. Abdul Njaidi akifuatilia kikao cha Kamati Tendaji ya chama kilichofanyika mjini Morogoro Desemba 18 na 19, 2020.
Tags
Habari